January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini

Fresha Kinasa,TimesMajiraOnline,Mara.

SERIKALI imeendelea kuimarisha sekta ya elimu katika Jimbo la Musoma Vijijini Mkoani Mara ambapo kwa sasa inajenga shule za Sekondari Mpya tatu Jimboni humo ikiwemo Butata Sekondari ambayo inajengwa Kijijini Butata Kata ya Bukima ambapo imeelezwa kuwa imepangwa ifunguliwe mwezi ujao, Februari 2025. 

Hayo yamebainishwa na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof.Sospter Muhongo kupitia taarifa yake iliyotolewa Januari 21, 2025 huku akimshukuru kwa dhati  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha nyingi za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni humo.

Kupitia taarifa hiyo Prof. Muhongo amesema kuwa, Serikali  inajenga sekondari mpya tatu (3) ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini, na kila ujenzi/mradi umepewa Shilingi Mil.  584. Huku akisema kuwa Ujenzi wa Butata Sekondari unaendelea vizuri.

“Butata Sekondari – Sekondari hii ni ya Kisasa inajengwa Kijijini Butata, Kata ya Bukima. Maabara tatu za masomo ya Sayansi, Chumba cha TEHAMA,na Maktaba ni miongoni mwa Miundombi muhimu  inayojengwa hapo.” amesema Prof. Muhongo.

Amesema mbali na Butata Sekondari ambayo inajengwa Kijijini Butata Kata ya Bukima ambayo ni Sekondari ya pili ya Kata hiyo pia Sekondari nyingine ya pili inajengwa na Serikali  Kijijini Kasomo Kata ya Nyamrandirira ambayo ni Sekondari ya amali na ya tatu ya Kata hiyo,  na Sekondari ya tatu inajengwa Kijijini Kurwaki kata ya Mugango ambayo ni Sekondari ya pili ya Kata hiyo na ni ya Kumbukumbu ya Prof. David Masamba.

“Ongezeko kubwa la Sekondari Jimboni mwetu, ambapo tunazo Sekondari 26 za serikali/ kata  Jimboni mwetu, Sekondari 2 za Binafsi(madhehebu ya dini Katoliki  na SDA.  Mwaka huu tunaongeza Sekondari Mpya sita,  High schools mbili za masomo ya Sayansi “amesema Prof. Muhongo.

Mbali ya sekondari hizo tatu zinazojengwa kwa kutumia fedha nyingi kutoka Serikalini,  Prof. Muhongo amesema  zipo nyingine tatu zinazojengwa kwa nguvu za wananchi na viongozi wao.

Ikiwemo katika  Kijiji cha Muhoji, Kata ya Bugwema  ambapo sekondari hiyo  ni ya pili ya kata hiyo  na imeanza kupokea michango kutoka Serikalini.
Ya pili ni Kijijini Nyasaungu, Kata ya Ifulifu ambapo  sekondari hiyo  ni ya pili ya kata hiyo ya tatu ni   Kisiwani Rukuba, Kata ya Etaro ambayo ni sekondari  ya tatu ya kata hiyo.

Naye magesa Julius Mkazi wa Kata ya Mugango Jimboni humo ameiambia Majira Online kwa njia ya simu kuwa,  Uwekezaji unaofanywa na Serikali katika sekta ya elimu ikiwemo kujenga shule Mpya,  maabara unalenga kuhakikisha kila mtoto anapata fursa ya kusoma karibu na nyumbani. Na pia amempongeza Prof. Muhongo kwa bidii, ufuatiliaji,  na ushiriki wake wa kuchangia fedha  katika kuhakikisha Jimbo hilo linakuwa na Wasomi wengi wenye faida kwa  Jamii na taifa kwa siku za usoni.Â