Na Aveline Kitomary,TimesMajira Online ,Dar es Salaam
UTUMIAJI wa kondom ni hatua muhimu zaidi kwa jamii kwani huweza kumkinga mtumijia na mgonjwa ya kuambukiza wakati wa ngono.
Kiwango cha utoaji elimu kuhusu matumizi ya kondom ni kubwa ambapo inasisitizwa kukinga magonjwa kama vile UKIMWI,Kaswende,Kisonono na magonjwa mengine ya kuambukiza.
Lakini sio hilo tu hata katika kampeni ya uzazi wa mpango matumizi ya kondom yanatajwa kama njia mojawapo y akumuepusha mtumiaji na mimba zisizotarajiwa.
Ni hatua muhimu zaidi kuzingatia matumizi ya kondom ambapo kundi kubwa la vijana elimu hiyo imewaingia vizuri.
Matumizi ya kondom ni hatua nzuri lakini je watumiaji wanaelewa njia ya kuhifadhi bidhaa hiyo isiweze kupoteza ubora wake?
Jarida la Majira ya Afya lilifanikiwa kupita kati maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam na kuzungumza na vijana ambao ni watumiaji wakubwa wa bidhaa hizo.
Katika mahojiano na vijana hao Mwandishi wa makala hii alipouliza kama wanaulewa kuhusu namna bora ya kuhifadhi kondom wengi wasisema hawajui.
“Mimi ni mtumiaji mzuri wa kondom lakini kuhusu uhifadhi hilo bado sijalijua ,huwa nanunua kondom na naweka hata mwezi mmoja na mara nyingi natembea nzno kwasababu naamini kuwa ni ulinzi kwangu.
“ninachokiangali katoka kondom ni muda wa matumizi ukiisha basi naitupata lakini kwa upande wa njia ya kuhifadhi naweza kuweka mfukoni nikatembea nayo au naweka kwenye wallet,”anaeleza John Koluwu kijana mwenye umri wa miaka 24.
Sio John tu hata Obedi anasema kwake kununua kondom na kukaa nayo muda mrefu ni jambo la kawaida na wakati mwingine kutembea nayo.
“Lazika geto kwangu niwe na kondom kwasababu wakati mwingine mpenzi wangu akija atataka tutumie hivyo naiweka kama akiba.
Alipoulizwa kuwa ni njia gani anatumia kuhifadhi kondom isipoteze ubora anasema “Sijui hilo kuwa kondo inaweza kupoteza ubora na hata namna ya uhifadhi wake siujui mimi nikinunua dukani tu basi.
“Lakini ninachoamini hata vijana wengi hawajui hilo lakini kuna wengine hata expire date hawaangali nafikiri kuna haja ya kulielewa hilo,”anasema Obedi.
Anaongeza “wakati mwingine utakuta wapo wanaoshea kondom moja akitumia huyu anaweza kumpa mwenzake akatumia hilo nilishawahi kusikia.
“alakini hata ukinunua unakuwa haumalizi kutumia zpte kwahiyo zinazobaki zinakaa na kuwa akiba.
HAZITAKIWI KUHIFADHIWA SEHEMU HIZI
Watumiaji wengi wa bidhaa za kondom hupenda kuzihifadhi katika mifuko ya suruali,droo za kabati au wallet zao kwa muda mrefu.
Hali ya kutembea nayo muda mrefu hasa kwenye mwanga wa jua na joto kali inaweza kuwa na hatari kubwa kwa mtumiaji.
Mchunguzi wa Maabara wa Mamlaka ya Dawa,Vifaa tiba na Vitendanishi (TMDA) Samson Mwambene anafafanua hapa “Tunahofu na kitu ambacho sio kizuri tukumbuke mazingira tunayotakiwa kuhifadhi kwanini uweke kondom kwenye waleti halafu unazunguka nayo mtaani na juani unazurura ni rahisi sana ikikutana na jua unatumia kondom haina ubora.
“Kuna wakati unakuta mtu analalamika kondom inapasuka kumbe ni namna anavyohifadhi mwingine ananunua leo anaenda kuiweka mahali sio salama inapata jua kondom inaharibika.
Kwa mujibu wav Mwambene anasema ni muhumi kuzinagatia uhifadhi wa kondom ili kulinda ubora wake na kufanya kazi kwa ufanisi.
Mwambene anasema kiwango cha juu cha joto kinachotakiwa katika uhifadhi wa kondom ni nyuzi joto 30 huku kiwango cha chini ikiwa ni nyuzi joto 10.
“Kiwango cha joto hakitakiwi kuzidi 30 sio vizuri kuweka kondom kwenye droo au sehemu yenye joto Unaweza kuhifadhi katika mazingira ya joto la chini 10 hadi 30.
“Unapoenda kununua kondom usiende kila mahali nenda sehemu kuna maduka ukiingia unahisi hali ya ubaridi unaona kimehifadhiwa vizuri kama unyevu uko juu itaharibu na pia kama joto iko juu itaharibika na hii ni kwa dawa na vifaa tiba pia.
“Kama kunakitu chenye madhara makubwa ni kutumia kondom na kufua na kuitumia tena madhara yake ni makubwa ukishatoa kwenye boksi kubwa halfu vidogo na kwenye pakiti haitakiwi kukaa muda wa dakika mbili,”anasisitiza.
Anasema mtu anapoifungua kondom anatakiwa aitumie muda huo huo na ikiachwa kwa dakika mbili inapoteza ubora wake.
“Tunashauri ukishafungua iwe tayari kwa matumizi sio unafungua ukaiweka hafu ukazunguka unakaja kuitumia au unatumia unaenda kusafisha na kuitumia tena.
“Tunasema kondom inatakiwa kuwa na mafuta kama utafua itakuwa kavu na itachanikana na kama haina mafuta oksijeni itakuwepo na ubora utakuwa haupo vizuri ,Hatushauri kabisa kutumia kondom ambayo imeshatumika,”anabainisha.
Anashauari kondom kuhifadhiwa sehemu salama.
“Kutembea na kondom ni kinga lakini unazingatia uhifadhi salama hicho ni muhimu isikutane na mwanga wa jua wala joto kali,”anasisitiza Mwambene.
ELIMU NI ENDELEVU
Kwa upande wake Meneja Mawsiliano na Elimu kwa Uma wa TMDA,Gaudensia Simwanza anasema mamlaka inaendelea kutoa elimu kwa watumiaji ili kujua namna bora ya kuhifadhi vifaa tiba ikiwemo kondom.
“Tunatoa elimu katika sehemu mbalimbali na hilo ni suala endelevu tunataka jamii kuwa na uelewa kuhusu hilo,”anasema Simwanza.
UPIMAJI UBORA KATIKA MAABARA
Mwambene anasema maabara ya TMDA inachunguza uwezo,ufanisi na ubora wa kondom za kike na kiume kabla ya kuingia katika soko.
Anasema zipo mashine za kisasa ambazo zinauweza wa kuchunguza kondom kwa kuangalia matundu,urefu,upana na kiwango cha mafuta kilichopo.
“Kuna mashine inaitwa Electrical leak tester(ELT) Kazi yake kwaajili ya kuchunguza mashimo madogo ambayo yanaweza yakawa kwenye kondom kwani zile kondom wakati wa uzalishaji unaweza kuenda tofauti vile ambavyo intarajiwa hivyo inatengeneza vishimo vidogo ambavyo hatuwezi kuziona kwa macho lakini wakati wa usafishaji hiyo inaweza kutokea na wakati wa utunzaji inaweza kutokea.
“Kwahiyo procees za uchunguzi zinaanza kufanyikia kiwandani inapozalishwa halafu sisi tunathibitisha ubora wa kile tunacholetwa kama inakidhibi ubora.
“ Kwasababu katika maelezo yao wanasema ni bora, hivyo tunathibitisha vipi sasa mashine hii inatusaida kuchunguza vitundu vidogo sana na yenye inauwezo wa kuchunguza kutumia umeme,”anaeleza.
Anasema katika mashine hizo kuna taa ambazo zinawaka kujulisha kama ni salama ua sio salama .
“Taa ikiwaka ya njano inaonesha kuna shida katika hiyo kondom na kukiwa hakuna shida zinawaka taa za kijani kuonesha kuwa hakuna tatizo.
“Tunaingiza maji kwenye kondom ambapo umeme unapita maji hayo sodium chloride ,Kama kondom haina tatizo la tobo itaonekana na kama inatatizo itaonesha sehemu Fulani inatatizo.
“Ili kuthibitisha kuwa toleo zima zilifeli au zimefauli katika kondom 315 tutakazo pima inatakiwa ziwe mbili tu zilizofeli kama ni zaidi ya mbili maana yake toleo zima linakuwa limefeli,”anabainisha.
Anasema toleo mara nyingi zinazalishwa kwa viwango tofautitofauti huku wengine ikiwa ni 500,000 na wengine chini ya 500,000.
“Kama ikotokea tukaruhusu kuingia mtaani ikiwa haijathibitishwa inaweza kuwa na madhara makubwa kwa jamii ,Wakati wa tendo msuguano unapotokea tundu litaruhusu kutoka majimaji ni hii itahatarisha maisha ya mtumiaji.
KUCHUNGUZA MAFUTA
Mwambene nasema kondom inaweza kuharibiwa na oksijeni hivyo inavyotengenezwa inawekwa mafuta (lubricant).
“Halafu wanaweka kwenye pakiti yakena wakati mwingine inatokea ile kifungashio walivyokuwa wanafungasha hawakufungasha vizuri kwahiyo yale mafuta yanatoka madhara ya kutoka yale mafuta yanasababisha vitu viwili .
“Kitu cha kwanza ile kondom itaanza kuharibika na adui wake mkubwa ni oksije itaanza kuharibu ile kondom .
“Cha pili ile lubricat ina potoka inaenda kuchafua vifungashio vingine hata kujua ni ipi inakuwa ni changamoto kwasababu mafuta yameshatoka na imeleta uharibifu kwenye vifungashio vingine
“mashine ya Visual Leak Tester (VLT) inaweza kutambua kama hii haijakaa vizuri, baada ya oksijeni kuharibu kondom na ukaenda kutumia inaweza kuchanikachanika kwasababu ubora haupo tena.
“Mfano mtu kaifungua kondom halfu kaiacha mahali iko kwenye pakage halafu baadae anatumia mafuta yanakuwa yametoka na kuwa kavu yale mafuta yanasaidia wakati wa tendo kulainisha na mafuta yakishatoka ikitumika inaweza kuchanika kwasababu ya msuguano itapasuka ,”anaeleza Mwambene.
Anasema Kazi ya mamlaka ni kuhakikisha bidhaa kuwa bora na mtanzani yuko salama hivyo inachunguzwa kwa umakini na wataalamu waliobobea.
“Bidhaa zilizoko katika soko pia zinafatiliwa ubora wake na kama tutakuwa na wasiwasi zitatolewa
Tunaangali kwamba kifungashio haina tatizo.
“Katika kuangali kiwango cha mafuta tunaangali sample 32 tu na katia hizo hazitakiwi kufeli zaidi ya mbili kama ikifeli toleo zima tunaliweka kwenye nkiulizo
“ kwani Matumizi ya kondom isiyo na ubora ni hatari sana kwani inaanza kumuangamiza mtu mmoja halafu familia na taifa, tukishapama maangamizi ya virusi au magonjwa ya zinaa au kuzuia mimba matokeo yake yanaenda mbali hivyo tuko makini zaidi katika kuchunguza.
“Kwahiyo inachunguzwa mara nyingi na watu tofauti tofauti hatuwezi kufanya uzembe kwasababu athari yake ni kubwa kwa watumiaji ,tunafatilia hadi mtaani kuwa watu wakilalamika kuwa hii inashida itakusanywa na italetwa kufanya uchunguzi halafu toleo husika litatolewa sokoni ,”anafafanua.
MUHIMU KUANGALIA MUDA WA MATUMIZI
Mwambene anasema Kifaa chochote inapopita muda wa matumizi huwa inakuwa na madhara endapo itatumiaka.
“Muda wa matumizi ukiisha inakuwa tayari sio salama kwa matumizi ni kitu muhimu sana mtu anatakiwa kunagalia muda wa matumizi kabla hajanunua bidhaa ,muda wa matumizi ukiwa umekaribia kama mfano umeenda kununua bidhaa Novemba na inakufa disemba nashauri kabisa usinunue kwanini ujiweke katika hatari .
Simwanza anasema kuna wakaguzi katika maeneo mbalimbali kuangalia bidhaa ambazo wanapima .
“Kama sampo iliyoharibika iko mtaani tutawasiana na mtengenezaji halafu itatafutwa nchi nzima na kuitoa soko ,Tunatoa taarifa kwa umma tunawaita tunawaeleza kuwa kuna toleo tumelitoa sokoni,”anasema Simwanza
More Stories
Ubunifu wa Rais Samia kupitia Royal Tour unavyozindi kunufaisha Tanzania
Rais Samia anavyojenga taasisi imara za haki jinai kukabilina na rushwa nchini
Rais Dk. Samia alivyowezesha Tanzania kuwa kinara usambazaji umeme Afrika