December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Sabaya aachiwa huru

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira

Hatimaye Mahakama ya Moshi Mkoani Kilimanjaro mchana huu imemuachia huru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya baada ya muda mfupi uliopita kukiri makosa yake yaliyokuwa yakimkabili.

Sabaya amekiri makosa yake kwa njia ya ‘plea bargaining’ ambao ni mchakato wa makubaliano/maridhiano maalumu katika kesi ya jinai kati ya Mwendesha Mashtaka na Mshitakiwa ambapo Mshitakwa anaweza kukubali kukiri kosa moja au zaidi katika makosa aliyoshitakiwa nayo ili apate nafuu katika kesi inayomkabili