Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online
KAMPUNI ya Bia ya Serengeti kwa kushirikiana na Chuo Cha Taifa Cha Utalii (NCT), wamezindua awamu ya pili ya programu ya ‘Learning for life’ katika tawi la NCT Arusha.
Imeelezwa kuwa, katika udahili kwa kipindi hiki kwa Arusha, zaidi ya vijana 150 wataandikiswa na kupata mafunzo ya vitendo yatakayolenga moja kwa moja ajira katika hoteli za kifahari na kawaida.
Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mkuu wa Chuo Cha Utalii (NCT), Dkt. Florian Mtey, aliongelea athari chanya za programu hiyo akisema”Programu hii imefungua milango mipya kwa wanafunzi wetu inawapa zaidi ya nadharia darasani kwa kuwapeleka kwenye mazingira zaidi ya kazi, jambo linaloongeza zaidi kujiamini na kuwapa uwezo wa kukidhi matarajio ya waajiri katika Sekta ya ukarimu na Utali, tunajitahidi kuendeleza ushirikiano huu na SBL hapa Arusha” amesema Dkt.Mtey.

Aidha imeelezwa kuwa, Mafunzo hayo ya muda mfupi yanatarajiwa kuanza, Septemba 22 mwaka huu na kuhitimishwa Novemba, 2025, huku gharama zote zikigharamiwa na SBL na wanafunzi wakigharamania malazi, chakula na usafiri.

Imesisitizwa kuwa, waombaji wote wanatakiwa kutuma naomba kabla ya Agosti 16, huku sifa za muombaji ni kuwa raia wa kitanzania, barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa au mwajiri, umri kati ya miaka 15 hadi 35, afya njema na elimu ya Cheti au fani ya Utalii na ukalimu.

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi