November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

SBL yazidi kuwekeza nchini

Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online

KAMPUNI ya Serengeti Breweries (SBL) wazalishaji wa vinywaji aina ya bia yaendelea kuwekeza nchini katika kuunga mkono juhudi za serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, wamezindua rasmi kinywaji kipya aina ya “Rockshore” jijini Dar es Salaam

Akizungumza na waandishi wa habari jana wakati wa uzinduzi wa kinywaji hicho Mkuu wa Uvumbuzi kutoka Serengeti Breweries Bertha Vedastus amesema kinywaji hicho chenye ladha ya tofauti ya bia nyingine ambayo itapatikana kwa Dar es Salaam kwanza lakini baadae kitasamba nchini nzima, pia kitauzwa kwa bei ya shilingi 2500 ambayo ni rafiki kabisa kuendana na hali ya uchumi.

“Kinywaji hichi ni cha kimataifa lakini kinazalishwa hapa hapa Nchini kwa viwango vya kimataifa ili kuhakikisha watu wanapata ladha halisi ya mchanganyiko wa nanasi na pensheni” alisema na kuongeza kuwa

“Serengeti tunazidi kuongeza nguvu mkubwa sana katika jamii kwa ajili ya kwenda kuwasaida kupata vipato kwenye njia tofauti tofauti”

Aidha, alisisitiza kuwa watu wasikae chonjo na wasiangalie tu “Rockshore” katika mpira lakini wamejipanga kuhakikisha wanatanua wigo mpana ukiachie mbali mpira, fashion na mziki ili kuzalisha fursa nyingi za ajira na watu kujikwamua kiuchumi.

Hivyo, aliwashauri wanasoka nchini kujiweka karibu na kampuni mbalimbali za kibiashara kwa lengo la kufanya nao matangazo kama ilivyo kwa wasanii endapo wanataka kujiongezea kipato mbali na mishahara wanayoipata kutoka kwenye klabu zao

Naye Mkuu wa Mauzo kutoka Serengeti Breweries Christopher Gitao alisema kuwa ni nafasi nzuri kwa watanzania ambao wanafanya kazi kwenye kiwanda hicho cha uzalishaji wa bidhaa hiyo mpya kwa kukuza uchumi wao na kuisaidia kampuni bidhaa hiyo kujulikana zaidi na ninaamini kila mtu atafurahi kinywaji hicho.

Kwa upande wake aliyekuwa mshindi wa ‘Miss Tanzania and Miss World Afrika 2005’ Nancy Sumari alisema uwekezaji huo utakuza mnyororo wa thamani nchini kwa kutengeneza ajira haswa kwa vijana na kuwasaidia wakulima na watu mbalimbali ambao watahusika kuhakikisha bidhaa hiyo inafika sokoni, pia kuwafikia walengwa ndani ya muda sahihi.