October 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

SBL yadhamini mashindano ya Waitara Trophy 2020

Na Penina Malundo, TimesMajira Online

TAKRIBANI wachezaji 150 wa gofu kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini wanatarajia kuchuana vikali katika mashindano ya kila mwaka ya mchezo huo maarufu kama ‘Waitara Golf Tournament’, yanayodhaminiwa na kinywaji cha Johnnie Walker (JW) kinachosambazwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL).

Mwaka jana, mashindano haya yanayojizolea umaarufu mkubwa, yalidhaminiwa pia na kampuni ya SBL kupitia bia yake ya Serengeti Lite.

Akitangaza udhamini huo, Mkurugenzi wa masoko wa SBL, Mark Mugisha alisema udhamini wa JW kwenye mashindano hayo unalenga kukuza na kuendeleza zaidi mchezo huo wa gofu ambao kwa sasa ni miongoni mwa michezo iliyoshika kasi hapa nchini.

“SBL kupitia kinywaji cha Kimataifa cha Johnnie Walker (JW) inayo furaha kuwa mdhamini wa mashindano ya Waitara Golf Tournament kwa mwaka huu kwani udhamini huu unaonyesha nia yetu ya kusaidia maendeleo ya michezo hapa nchini,” amesema Mark.

Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa, wanatarajia kuona ushindani mkali katika mashindano hayo ambayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka kuanzia mwaka 2006, ili kudhihirisha kuwa kasi ya mashindano yaliyoanza muda mrefu zaidi hapa Tanzania inaongegeza zaidi kupitia udhamini wa JW.

“Wakati tukishereheka miaka 200 tangu kuanza kutengenezwa kwa JW ambayo kwa sasa ni Wisky namba moja ulimwenguni, tunayofuraha kusafiri katika miaka yote hii tukiendelea kuwa imara na katika ubora ule ule,” amesema.

Johnnie Walker ni moja kati pombe kali zenye ubora wa hali ya juu na hadhi ya kimataifa. Kinywaji hiki kina jumla ya aina tano ambazo zimeshinda tuzo za ubora wa kimataifa. Aina hizo ni pamoja na JW Red Label, JW Black Label, JW Green Label, JW Gold Label, na JW Blue Label kila moja ikiwa na historia yake ya kipekee.

Akizungumzia udhamini huo, Mwenyekiti wa klabu ya Gofu ya Lugalo Bregedia Generali Mstaafu Michael Luwongo ameishukuru SBL kupitia JW kwa kukubali kudhamini mashindano hayo na kuyataka makampuni mengine kujitokeza kusaidia mchezo wa gofu.

“Tunaishukru sana kampuni ya SBL kwa muendezo wao wa kufadhili mashindano hay ana mchezo wa gofu kwa ujumla. Kwa sasa tunaweza kusema SBL ndiyo mdhamini mkubwa wa mashindano haya,” amesema Bregedia Jenerali Luwongo.

Lakini pia ametoa wito kwa wachezaji wa Golf nchini kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika mashindano hayo makubwa ambayo yataanza kutimua vumbi rasmi Novemba 21 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Faraji Mnyepe.

Bregedia Jenerali Luwongo amesema kuwa, klabu yao imejiandaa vizuri kwa ajili ya kuendesha mashindano hayo ikiwa ni pamoja na maboresho makubwa ya viwanja kwa sehemu zote zilizokuwa na utata lakini pia kutakuwa na waangalizi viwanjani (marshals) kwa ajili ya kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa na zawadi kutolewa kwa washindi wa madaraja yote.

“Mashindano haya ni kwa ajili ya heshima kwa muasisi wa Klabu Jenerali George Waitara Mstaafu ambayo hufanyika Novemba kila mwaka lakini pia shindano hili ni la siku moja ambalo litatanguliwa na shindano la wachezaji wa kulipwa watakaocheza siku ya Ijumaa huku wachezaji wa ridhaa maana ya Div A, B, C, Seniors na Ladies watacheza siku ya Jumamosi Novemba 21 na safari hii watoto hawataruhusiwa kutokana na wadhamini wa shindano hili ni kampuni ya SBL hivyo kinyume na malezi ya watoto,”.

Mashindano hayo yatajumuisha wachezaji kutoka klabu zote za hapa nchini ikiwemo Moshi Club, Arusha Gymkhana, Mufindi Club, Morogoro Gymkhana, Dar es Salaam Gymkhana, Sea Cliff Golf Club Zanzibar, Kili Golf na TPC Golf Club.

Nahodha wa klabu hiyo, Kapteni Japhet Masai amesema kuwa mashindano hayo ni ya Mikwaju ya juu ya Neting na sio grossing hivyo mshindi wa jumla atapatikana kwa mikwaju ya jumla ukiondoa madhaifu ya kimchemzo.