Na Mwandishi Wetu,timesmajiraonline,Dar
WAGONJWA wengi wa saratani hufariki dunia kutokana na kuacha tiba sahihi hospitalini na kujitibu kienyeji kwa watu wasio na ujuzi wa ugonjwa huo.
Hayo yamesemwa na Mratibu wa Huduma wa Hospitali ya Besta, Dkt. Ismail Dauda kufuatia kauli ya Serikali kuwa ni asilimia 31 tu ya wagonjwa wa saratani nchini wanatibiwa hospitalini.
“Kwa sasa ni asilimia 31 tu ya wagonjwa wa satarani wanatambulika kupata matibabu lakini kuna asilimia 69 ya wag-onjwa hawatambuliki wanapata wapi matibabu,” alisema Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dkt. Mark Mseti kwenye maadhimisho ya Siku ya Mashajaa wa Saratani Duniani, yaliyofanyika kitaifa Jijini Dar es Salaama mwishoni mwa wiki.
Dkt. Mseti alikuwa akisoma hotuba ya Waziri wa Afya, Jenista Mhagama, ambaye alikuwa ni mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo, alihimiza jamii kuhamasisha wagonjwa wasaratani kutibiwa hospitalini.
Mratibu wa Huduma Hospitali ya Besta alisema wagonjwa wengi wanapojikuta katika hali mbaya huenda hospitali jambo ambalo linakuwa ni vigumu kupona.
“Ninachoihamasisha jamii ni kuamini kuwa mgonjwa yeyote wa saratani akifika hospitalini katika hatua za awali za ugonjwa hutibuwa na kupona kabisa,” alisema Dkt. Dauda akifafanua:
“Mfano katika hospitali yetu ya Besta, tuna vifaa vya kisasa ambavyo huweza kubaini haraka hali halisi ya ugonjwa wa saratani. Pia tuna vifaa vya kisasa vya tiba ambavyo vinawezesha mgonjwa kutibiwa vyema na kupona haraka.”
Alionya kuwa wagonjwa wengi hudanganyika kupata tiba zinazotangazwa kiholela mitaaani kwa wanaodai ni tiba mbadala lakini wengi wao hujikuta hawaponi na hali ya mgonjwa kuwa mbaya zaidi.
Akielezea kuhusu hali halisi ya saratani nchini, Dkt. Mseti alisema takwimu zinaonesha kila mwaka kuna visa vya satarani zaidi ya milioni moja duniani. Kwa Tanzania zaidi ya visa 44,000 vya saratani vinatokea na waathirika wakubwa ni kinamama.
Alizitaja saratani zinazoongoza nchini kuwa ni ya shingo ya kizazi, matiti na tezi dume.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Shujaa Foundation, Gloria Kida, aliitaka serikali kuweka mkakakati maalumu wa kutatua kero za wagonjwa wa saratani ambazo pia zinaweza kuwa ni sababu ya wengi kutopata huduma sahihi hospitalini.

Alitoa mfano wa wawagonjwa wanaosafiri kutoka mikoani kupata tiba hospitali ya Saratani ya Ocean Road hujikuta wanapata shida ya eneo la kulala kutokana na kushindwa kumudu gharama za nyumba za kulalala wageni.
Alishauri Serikali kuangalia uwezekano wa kujenga hosteli maalumu ya wagonjwa wa saratani iambayo ama watakaa bure au watatozwa gharama wanazoweza kuzimudu.
Mbali na hilo, alisema ugonjwa wa saratani huambatana na changamoto kubwa kwenye familia ikiwa pamoja na kusemwa vibaya na kutengwa.
“Wapo wanaotakiwa kupata matibabu kwa muda mrefu, hii hali inakuja na changamoto kwa wagonjwa, wapo wanaofikia kwa ndugu, muda mwingine ndugu wanachoka na kuanza
kuwatenga wagonjwa.
“Kuondokana na changa- moto hii, serikali ijenge hosteli kwa ajili ya wag- onjwa wanaotoka mbali kuja kupata matibabu Ocean Road, iwe ya bure au hata kwa kuchangia kidogo,” alisema Gloria na kuongeza.
“Wengi wanafahamu wakipata saratani wamepata kibali cha kifo, imani ambayo si sahihi. Elimu haijawafikia watu, wengi hasa vijijini. Kuugua saratani si kifo. Wengi wanatibiwa na kupona.”
changamoto zinazowakabili wagonjwa na imetoa maagizo kwa Ocean Road kushirikiana na wadau wengine kutatua changa- moto zilizopo.
More Stories
Sheikh Ponda kutua rasmi Act Wazalendo
Puma Energy Yazindua Mradi wa Umeme wa Jua kwa Kiwanda cha Alliance One
Taasisi ya Jalaram Seva Mandal yatoa msaada kwa Watanzania