Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online.
DarKAMPUNI ya Bima ya SanlamAllianz, imetoa shukrani kwa mawakala wake kwa mchango waliotoa wa kukuza biashara ya bima.
Akizungumza wakati wa halfa iliyofanyika Novemba, 28,2925 jijini Dar-es-Salaam, Meneja mkuu wa biashara na mawakala, Geofray Masige amesema kuwa, kampuni hiyo ya SanlamAllianz, mbali na kutoa pongezi kwa mawakala hao, pia imeona ni vyema kutumia nafasi hiyo kuwatambulisha mawakala waya.
“Mnamo Septemba 2023, kampuni ya Sanlam bingwa wa huduma za bima barani Afrika na Allianz ambao ni miongoni mwa makampuni makubwa zaidi ya bima duniani, ziliungana kutengeneza kampuni kubwa ya kifedha isiyo ya kibenki barani Afrika, inayojulikana kama SanlamAllianz.

Muungano huu umeunganisha uzoefu wa pamoja wa zaidi ya miaka 200 barani Afrika na duniani, ambapo Malengo yetu ni kutoa huduma bora zaidi, kuunda bidhaa zinazokidhi matarajio ya wateja na kujenga jamii inayopata ulinzi wa maisha, fedha, mali na mafanikio endelevu”, amesema Masige.

Aidha amesema kuwa, kufuatia uzinduzi rasmi wa chapa mpya mwishoni mwa mwezi wa kumi, Sanlam General Insurance imeungana na Jubilee General Insurance kuunda SanlamAllianz General Insurance Tanzania na kubadili jina kuwa SanlamAllianz Life Tanzania.
Imeelezwa kwa sasa, SanlamAllianz General Insurance ina takribani mawakala 300 nchi nzima, lengo likiwa kuwafikia mawakala 350 ifikapo mwaka 2026.

More Stories
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI