January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Sangeni International kinara wa uwakala elimu ya juu nchi za nje

Na Bakari Lulela, TimesMajira Online, Dar

SANGENI International ambao ni wakala wa elimu ya juu nje ya nchi imejipambanua kuendelea kutoa huduma bora kwa wanafunzi watakaotaka kwenda kusoma elimu ya juu nje ya nchi kupitia kampuni hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa maonesho ya 16 ya vyuo vikuu,Sayansi na Teknolojia yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam,yakiwa chini ya uratibu wa Tume ya Vyuo vikuu Nchini (TCU) Meneja Mkuu wa Wakala huo Bw. Jadian Saimon alisema kwamba Sangeni Inaternational inawasaidia wanafunzi wanatazania kusoma nje ya nchi na kutimiza ndoto zao.

Meneja Mkuu Jadian Saimon wa wakala wa kuwatafutia nafasi za masomo wanafunzi  nje ya nchi Sangeni International, akielezea huduma wanazozitoa kwa waandishi wa habari
(hawapo pichani) waliotembelea banda hilo katika Maonesho ya 16 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia mkoani Dar es
salaam.

Saimon amewaambia wanahabari kuwa kampuni hiyo imekuwa ikiwaunganisha wanafunzi raia wa Tanzania na vyuo mbali mbali duniani hususani vyuo ambavyo vianatoa kutoa ofa za punguzo la ada hadi asilimia 50 na zenye uhusiano na vyuo vikuu vya nchini India nakutumia fursa hiyo kuwataka wazazi au walezi kuchangamkia fursa hiyo katika kipindi hiki cha udahili wa wanafunzi wa kujiunga na elimu ya juu.

“Katika Maonesho haya ya 16 ya Elimu ya Vyuo Vikuu 2021 yanayofanyika kuanzia Julai 26 hadi 31 katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Sangeni International ikishirikiana na Manipal Academy of Higher Eucatio Dubai Campus kupitia shughuli hii ya maonesho chuo kinatoa punguzo la ada ya mwaka asilimia 30 kwa wanafunzi mwaka wa kwanza na asilimia 25 kwa digrii ya pili wale tu watakaojisajili na chuo, “ amesema Meneja huyo.

Mwakilishi wa Sangeni Internationl akimsiiliza mwananchi aliyetembelea banda lao katika maonesho 16 Elimu ya juu ya Sayansi na Teknolojia Mnazi Mmoja mkoani Dar es Salaam.

Nakuongeza kwamba “Wanafunzi hao pia watapata tiketi ya ndege kuelekea mji wa Dubai na watapokelewa uwanja wa ndege na kufikishwa kwenye malazi ya chuo na watalipiwa bima ya afya kubwa kwa mwaka wa kimasomo wa mwanzo”.

Saimoni amEsema kwamba Sangeni International inahakikisha inashirikiana na chuo kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata kazi za muda za kulipwa wakati wakiwa masomoni Dubai kwa kuwakabidhi vibali au vyeti vya “No Object Certificate” (NOC) hivyo hali hiyo itawasaidia wanafunzi kupata kipato cha kujikimu kipindi cha masomo yao.