December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Samia Queens wazindua wimbo mpya

Na Mwandishi Wetu, TimesmajiraOnline, Dar

WANAMUZIKI wa kike nchini Tanzania, Samia Queens wamezindua wimbo wao maalumu kwa ajili ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa kila tarehe 8 Machi.

Uzinduzi wa wimbo huo ulimefanyika juzi katika ofisi ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar Es Salaam, kwenye Mkutano wa Katibu Mkuu wa Jumuiya wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania UWT Jokate Mwegelo.

Hata hivyo katika uzinduzi huo Jokate aliwataka wanawake wote nchini kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kila jambo.

Miongoni mwa Wasanii wanaounda kundi hilo ni, Lady Jaydee, Zuchu, Nandy, Shilole, Lulu Diva na wengine wengi.