Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Zanzibar
RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa taasisi za kiserikali na sekta binafsi kufanya jitihada za kuhakikisha wanawake wanapata nafasi na kusikika kwenye maamuzi mbalimbali nchini.
Rais Samia amesema hayo leo kwenye mkutano wa wanawake walio katika sekta ya fedha uliofanyika visiwani Zanzibar.
Aidha, Rais Samia alisema ushiriki wa wanawake kwenye ngazi za maamuzi ni suala jumuishi na endelevu, hivyo halipaswi kuchukuliwa kama la kimapinduzi au la serikali pekee.
Rais Samia amebainisha kuwa lengo ni kuhakikisha masuala yanayowahusu wanawake ambayo wafanya maamuzi wengine wanaweza wasiwe na uelewa nayo yanapata nafasi kwenye meza ya maamuzi.
Hali kadhalika, Rais Samia alisema pamoja na kuongeza ushiriki wa wanawake kwenye ngazi za maamuzi, lazima pia kuweka nguvu kubwa katika kuwainua wanawake kiuchumi.
Kwa upande mwingine, Rais Samia amewataka wanawake kujipanga na kufikia malengo yao kwa vitendo.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi