Na Mwandishi Wetu, Timesmajiraonline,Dar
RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa zawadi ya sh milioni 700 kwa timu ya Taifa (Taifa Stars), kufuatia ushindi wao wa bao 1-0 dhidi ya wageni wao Guinea, katika mchezo wa mwisho wa kuwania kufuzu fainali za AFCON mwaka 2025.
Katika mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jana,Stars ilishinda bao 1-0 lililofungwa na Simon Msuva na kukata tiketi ya kufuzu fainali hizo mwaka 2025.
Akizungumza baada ya kukamilika kwa mchezo huo uliohudhuriwa maelfu ya mashabiki, Waziri wa Utamadunia Sanaa na Michezo, Damas Ndumbaro, alisema Rais Samia ametoa fedha hizo kama sehemu ya kupongeza mchango wa wachezaji na benchi lote la ufundi la Taifa Stars.
“Rais Samia anathamini kazi kubwa na mchango uliotelewa na wachezaji hao, hivyo ameamua kutoa kiasi hicho cha fedha kama zawadi ambapo tayari zimeingizwa kwenye akaunti ya Wizara ya mchezo,”Alisema Ndumbaro.
Katika hatua nyingine, Waziri Ndumbaro alisema wachezaji wa Taifa Stars wamealikwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baadaye mwezi Febuari, mwaka 2025.
More Stories
15 wajinoa Juventus,akiwemo mtoto wa Mwenyekiti wa CCM Mbeya
Za Kwetu Fashion Show, yawapaisha wanamitindo nchini
TCAA yaadhimisha siku ya usafiri wa anga Duniani kwa kushiriki mbio za Marathon UDSM