January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Sambaza upendo yatoa msaada msikiti Shia Ithna Sheria

Na Bakari Lulela, Timesmajira Online

Taasisi ya Sambaza Upendo imetoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo nguo,viatu kwa wahitaji msikiti Shia Ithna Sheria uliopo Kigogo jijini Dar-es-Salaam.

Akizungumza jijini Dar-es-Salaam ,katika hafla ya utoaji wa misaada hiyo,Mratibu Mkuu wa taasisi hiyo Askofu IKomba Banza amesema kufanya yaliyo mema na kuwaonea huruma wengine ni mambo yanayompendeza Mungu.

Askofu Banza amesema kuwa taasisi hiyo iliazishwa mwaka 2018,walikuwa wakitoa huduma ya kuwasaidia watu wanaoishi katika mazingira magumu wakiwemo yatima, wajane na wazee.

“Mbali na utoaji wa huduma za kiimani kwenye nyumba za ibada sambaza upendo tunawawezesha vijana mbalimbali kuachana na matumizi ya dawa za kulevya,bangi na wanaojipatia fedha kwa kuuza miili yao,”.

Pia ameeleza kuwa nia ya taasisi hiyo ni kuona watanzania hususani vijana wa dini zote Wakristo na Waislamu wanapata mafunzo ya kiufundi ili yawasaidie kuondoa changamoto mbalimba

Hata hivyo ameeleza changamoto mbalimbali zinazoikabili taasisi hiyo ni pamoja na ukosefu wa usafiri kwa ajili ya kuzunguka maeneo mbalimbali.Bado wanahitaji eneo kwa ajili ya kuweka kituo cha kulelea watoto na jamii inayoishi katika mazingira magumu, sehemu ya kufungua viwanda vidogo na eneo la shamba kwa ajili ya kilimo.

Kwa upande wake Sheikh wa msikiti huo Ahmed Abdi amesema ni muhimu kuwasaidia wahitaji kama vitabu vya dini vinavyoelekeza

Nae Mwanzilishi wa taasisi hiyo Askofu Dkt. Leonard Ntibanyiha amesema  kuwa kikundi hicho kinajukumu la kuwasaidia vijana walio katika mazingira magumu,wajane na wazee.

Amesema alipata maono ya kuanzisha jambo hilo mwaka 2018 baada ya kupata ndoto akiwa amelala usingizini.

Askofu huyo ametunga kitabu chenye kutoa mwanga wa kuwahudumia jamii iliyokosa usaidizi.

Alisema sambaza upendo wanategemea kuendesha huduma yao Septemba 21,mwaka huu wanategemea kuendesha huduma hiyo ya utoaji misaada kwa wahitaji pamoja na neno la Mungu Mbezi Luis jijini Dar-es-,Salaam.