December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Sakata la Harmonize, Jeshi la Polisi latoa tamko

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linaendelea kuchunguza tuhuma za kusambaa picha za utupu zikimuhusisha Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Rajab Abdul Kahal maarufu kama ‘Harmonize’.

Akizungumzia hilo leo, Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema, hadi sasa wamehojiwa watu watano kuhusiana na sakata hilo na wapo nje kwa dhamana.

Kamanda Mambosasa aliwataja Watuhumiwa hao ni Frida Kajala Masanja (36), Paula Paul Peter (18), Raymond Mwakyusa maarufu RayVanny (27), Claiton Revocuts maarufu Baba Levo (34), Catherine John na Juma haji (32).

“Watuhumiwa hawa wote walikamatwa, wakahojiwa na kwa vile dhamana ipo wazi wapo nje kwa dhamana na taratibu za upelelezi zinaendelea zikikamilika jalada litaenda kwa Wakili Mkuu wa Serikali na kama akiona kuna jinai watafikishwa Mahakamani,” amesema Kamanda Mambosasa.