Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline,Tanga
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani nchini amefungua Kikao cha Wenyeviti wa Usalama Barabarani Tanzania Bara katika Ukumbi wa Mikutano wa Mtendelee Hoteli Mkoani Tanga.
Akizungumza Machi 7, 2024 wakati wa akifungua Kikao hiko Sagini amesema kuwa, kupitia Baraza la Usalama Barabarani na kamati zake zinajukumu la kumsaidia Mhe. Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania kuongoza nchi katika Sekta ya Usalama barabarani.
“Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya kazi kubwa ya kuimarisha Bajeti za barabara mpaka za Vijijini na kuendelea kuboresha miundombinu hii tunayoitumia mpaka Mijini hivyo tuna jukumu la kufanya kuhakikisha anapata faraja lakini ikiwa kinyume chake itakuwa ni kazi bure kwani ndio kiongozi wa kwanza kutenga bajeti kubwa katika sekta ya barabara na haijawahi tokea hapo kabla” Alisema Mhe. Sagini
Kwa upande wake Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Naibu Kamishna wa Polisi DCP Ramadhani Ng’anzi alimuhakikishia Naibu Waziri kuwa, wanashirikiana vema na Sekta zote zinazosimamia barabara pamoja na mamlaka za usafirishaji ndio maana ajali za mabasi zimepungua kwa sababu mabasi yote yanafuatiliwa katika mfumo maalumu ili kuhakikisha abiria wanasafiri na kufika salama ambapo pia madereva wote wamesajiliwa na LATRA na ni wajumbe katika Baraza la Usalama Barabarani.
Naye Mwenyekiti wa Wenyeviti Idd Azan ambaye ni Mjumbe katika Baraza hilo aliipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa usimamizi mzuri na kuruhusu magari ya abiria kusafiri usiku kwani ilikuwa kama haiwezekani kutokana na fikra za wengi zilikuwa zinajua ajali zitazidi ila kupitia maelekezo na ufuatiliaji wa Viongozi mpaka sasa abiria wanazidi kupenda safari za usiku.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi