December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Mbung'o

Rushwa ya ngono vyuo vikuu nchini yaitikisha TAKUKURU

Na Joyce Kasiki,times major a online,Dodoma

MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Mbung’o, amekiri kuendelea kuwepo changamoto ya rushwa ya ngono katika vyuo vikuu nchini.

Brigedia Mbung’o ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma katika warsha ya wadau iliyojadili matokeo ya utafiti wa rushwa ya ngono katika taasisi za elimu ya juu nchini.

Amesema rushwa ya ngono bado ni tishio kwa jamii hivyo suala hilo linapaswa kutiliwa mkazo kwa nguvu zote katika kulikemea.

Amesema wao wakiwa kama wenye dhamana ya kusimamia haki kwa kupinga vitendo vya rushwa kwa namna yoyote ile wamejipanga kushughulikia kero ya rushwa ya ngono kwa kuweka madawati ya malalamiko Katika kila mikoa.

Brigedia Mbung’o amesema madawati hayo yameonesha kuzaa matunda ambapo jumla ya mafaili 23 ya kesi yamefunguliwa huku bado yakiwa yanashughulikiwa kwa kina.