Na Mwandishi Wetu, Pretoria, Afrika Kusini
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametumia sehemu ya hotuba yake akihitimisha ziara yake nchini Afrika ya Kusini kusifu mafanikio ya filamu aliyoshiriki kunadi utalii, biashara na uwekezaji nchini Tanzania ya “Tanzania; The Royal Tour” kuwa imeleta watalii wengi zaidi katika Taifa hilo la Afrika Mashariki lenye vivutio lukuki.
Akizungumza wakati wa kikao chake na Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, wafanyabiashara na watendaji kutoka nchi hizo mbili, Rais Samia, amewaalika wawekezaji kuwekeza nchini Tanzania katika sekta mbalimbali huku akisisitiza kuwa sekta ya utalii inahitaji hoteli nyingi zaidi hivyo wachangamkie fursa hiyo.
Mkutano huo wa Pili wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (Bi-National Cooperation) kati ya Tanzania na Afrika Kusini umehitimishwa leo Machi 16, 2023 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Afrika ya Kusini (CSIR ICC).
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria