December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rose Ndauka awapa makavu wanaomfuatilia maisha yake

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MSANII wa filamu na Mjasiriamali hapa nchini Rose Ndauka, amewapa makavu wale wote wanaomfuatilia maisha yake katika page yake ya Instagram hasa anapoposti kitu chake, waache mara moja ili waweze kufuatilia mambo yao na wafanye makubwa kulinganisha na yeye.

Akitoa makavu hayo kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram Rose amesema, anashangaa kuona watu wakitoka na mapovu hasa baada ya kuposti picha alipomtembelea Bibi yake Kijijini kwa ajili ya kudhuru kwenye kaburi la Baba yake.

“Naona watu wanatokwa na mapovu mengi kutokana na post nilizopost nyuma, hivi mbona watu wa Instagram mnapenda sana kudanganywa mlitaka tukapige picha gorofani ndio tuseme kwa bibi yetu, lini tuliwaambia sisi ni Mabilionea tuna uwezo wa kuwajengea familia nzima na hata kama tunazo tunanya kwa nafasi sio sababu ya watu na hilo halituzui sisi kuishi vile tupendavyo.

“Kwa kifupi wale wanaochonga sana, ohooo jengeni nyumba mara wekeni plasta wakati kwa bibi na wazazi wenu kijijini hata vyoo hawana wanajisaidia chini ya mti fateni ya kwenu kwa hii page yangu ni yanayonihusu tu na vile nipendavyo. Nadeka zangu kwa bibi leo, wewe mwenye hela kajengee ukoo wako wote,” amesema Rose Ndauka.