January 24, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Roma amtumia ujumbe mzito mkewe

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MSANII wa HipHop hapa nchini Roma Mkatoliki, amemtumi ujumbe mzito mkewe, baada ya kutimiza miaka mitano ya ndoa yao na kutakiana kheri kwa walipo na wanapoelekea.

Akitoa ujumbe huo kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram Roma amesema, amekumbuka miaka 11 iliyopita jinsi walivyokuwa wanatakana yeye na mkewe mpaka wakafikia kufunga ndoa.

“Nakumbuka kipindi kile miaka zaidi ya 11 iliyopita, ulivyokuwa unanitongoza nakukatalia, ukanitongoza mara ya pili nikakuchomolea ukawa unalia sanaa daaaah, mara ya tatu nikaja kukuonea huruma nikakukubalia tukaanza mahusiano, leo tuna miaka mitano kwenye ndoa yetu hakika Yehova ni mwaminifu

“Huku kila nikitaka kuku-cheat inanijia ile sura yako ukilia mbele ya waandishi wa habari kipindi nimetekwa, ikinijia tu basi hisia zote zinakata naishiwa nguvu nawafukuzia mbali wazungu, navuta shuka nalala peke yangu, Mungu aendelee kudumisha ndoa yetu usiache kuniombea Shetani asije akanihadaa nami nafanya hivyo pia” ameandika Roma.