December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Roma ampa makavu Nikki Mbishi

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MKALI wa hiphop hapa nchini Ibrahim Musa maarufu kama ‘Roma Mkatoliki’, amempa makavu msanii mwenzie Nikki Mbishi kuwa punguze chuki jambo ambalo linamaliza kipaji chake.

Akimpa makavu hayo kupitia kwenye Ukurasa wake wa Istagram, Roma amemtaka msanii huyo kubadilika kwa kuacha kuwafuatilia wasanii wenzake badala yake ajijenge yeye mwenyewe ili mziki wake uweze kukua.

”Niki!! punguza chuki, chuki zinakimaliza kipaji chako, fanya muziki acha makasiriko kwa wasanii wenzako, acha chuki, haikujengi inakubomoa kila leo.
Kuna wakati unasngizia hiyo life style yak ndio hiphop, sio kweli Hiphop haitufundishi chuki, hiphop ni love& peace. Utamaduni wa hiphop unatufundisha umoja.

“Miaka inakwenda mzee mwaka wa 10 huu unatumia some Approach kwenye game, badilika, watu wamekua sasa, wanafocus kwenye majukumu ya familia, wanalea watoto, wanaifanya hii Game biashara, wana-Squash Beef, Wana-Unit’ ‘Keep Ya’ Head Up Son!!’. Usirudishe watu kwenye maisha ambayo washayapitia, muda hautoshi, kua mzee, fanya muziki wako kwa njia yako mwenyewe pasi kuzungumzia watu.
“Wasiokuzungumzia au kukujibu ili uje ufurahie matunda ya muziki wako kimpango, tengeneza conteny ya muziki wako, peleka sokoni ikipendwa na wengi watanunua tu. Shabiki hahitaji umshikie bunduki ndio akupende, kwa hiyo heshimu na wakumbatie wachache ulionao, focus kuwatengeneza wengine wengi, kumbuka wengi ni Mutual fans, kwa hiyo zingatia tu content zako.

“Wakati mwingine unaowawekea chuki, wao wanajitafuta kwa njia zao pasi kuku-bother wewe, Na pengine hata wao hawajafanikiwa kiivo, unawawekea chuki bure, tabia za kichawi hizo, wakatoliki hatufundishwi hivo!! badala msapotiane kuijenga game pamoja kama wenzenu, nyie mnataka tuvutane tuanguke wote ‘Then You Come Out’ na kujinadi, wewe ni mwana wa hiphop kaka huu ni mwaka 2021. Tumeshatoka huko kwenye hizo zama.

“Una Mu-Attack kila msanii, una matatizo gani?, leo huyu hajui, kesho yule anabebwa. Huheshimu mkubwa wala mdogo, unamchukia hadi mtoto ambaye hajazaliwa. Hiyo sio hiphop, huwezi kuwa unajua kila kitu, huwezi kuwa uko sahihi kila kitu, punguza U-Much Know!!,”ameandika Roma Mkatoliki.