Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
KATIKA kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu sita ,bajeti ya kununua vifaa tiba imeongezeka kutoka shilingi bilioni 35 wakati Rais Samia Suluhu Hassan anaingi madarakani hadi kufikia shilingi bilioni 181 inayotengwa sasa.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri ,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Zainabu Katimba kufuatia swali la Mbunge wa Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi ambaye alitaka kujua mkakati wa serikali wa kusaidia wananchi wa kata ya Oldmoshi Mashariki wanaotibiwa katika zahanati ya Fumvuvu kupata huduma bora za afya kwa kununua vifaa tiba na upatikanaji wa maabara.
“Zahanati ya Fumvuvu kata ya Oldmoshi Mashariki ina uhaba mkubwa wa maabra na vifaa tiba ,serikali ina mkakati wa kusaidia wananchi upatikanaji wa maabara na vifaa tiba ili waweze kupata huduma bora za afya.
Katimba amesema,kufuatia kuongezeka kwa bajeti ya kununua vifaa na vifaa tiba zahanati hiyo itafikiwa.
“Namuhakikishia Mheshimiwa Mbunge kuwa fedha zipo kwa ajili ya kununua vifaa na vifaa tiba .” amesema Katimba
Ametumia nafasi hiyo Kumuagiza Mganga Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na Mganga Mkuu wa wilaya ya Moshi kumsimamia Mkurugenzi ili kuhakikisha vifaa hivyo vinapatikana.
Kuhusu jengo la maabara Katimba amesema Serikali inaendelea kuhakikisha inaboresha miundombinu katika sekta ya afya kwa kuendelea kujenga majengo ya kutolea huduma za afya msingi zikwemo zahanati
“Serikali kupitia mapato ya ndani na serikali Kuu inaendelea kuimarisha huduma za afya msingi na itafika katika jimbo la Moshi vijijini.”amesisitiza Katimba
More Stories
Samia awataka wanahabari kutanguliza uzalendo mbele
UAE yamtunuku Rais Samia Medali ya juu kabisa
Rais Samia amteua Mkurugenzi Mtendaji TANESCO