Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online, Dar es Salaam
WANANCHI zaidi ya Elfu Tatu waliyotembelea banda la Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini –RITA- wamesajiliwa kwenye mfumo ambapo kati yao mia mbili na hamsini tayari wamepatiwa vyeti vya kuzaliwa.
Hayo yamesema jana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhibiti (Rita), Frank Kanyusi alikuwa akipokua akishuhudia wananchi wengi waliyojitokeza kwenye banda hilo ambalo lipo kwenye ushiriki wa Monesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa maarufu Sabasana yanayoendelea kufanyika Jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu huyo wa (Rita) alisema huduma waliyoipa kipaumbele kwenye maonesho hayo ni kwa wananchi mbalimbali ambao kabisa hawana cheti cha kuzaliwa ndiyo wanaopewa nafasi ya kusaidiwa kupatiwa cheti hicho.
Jumuku la (Rita) ni kutoa huduma bora kwa wananchi wake hasa ikiwemo cheti cha kuzaliwa, kwa hivyo kupitia maonesho haya ya Sabasaba tumetumia nafasi hiyo ya kuwasaidia Watanzania wanaofika kwenye banda letu waweze kusaidiwa kwa haraka kupata cheti cha kuzaliwa kwa urahisi alisema Kanyusi.
Aidha amesema (Rita) inaendelea kutoa elimu zaidi kwa wananchi ikiwemo suala la kusajili kutoa vyeti kwa wananchi wenye sifa, kuendelea kutoa elimu kuhusu mirathi na kuandika wosia.
Taasisi hiyo pia imewataka wananchi ambao wanatumia vyeti vya zamani vilivyopitwa na wakati, wameombwa warejeshe vyeti hivyo kwenye ofisi yoyoteya (Rita) iliyopo kwenye wilaya wanazotoka ili kusudi Taasisi hiyo iweze kufanya utaratibu wa kuwapatia vyeti vipya vinavyoendana n a mfumo waliyokuwa nao.
Natoa rai kwa watanzania wenzangu ambao wana vile vyeti vyenye mfumo wa zamani ambavyo ni virefu, waturejeshee kwenye ofisi zetu na sisi tufanye utaratibu wa kuvitambua na kuwapatia vyeti vipya vinavyoendana na mfumo wetu wa kisasaalisema Kanyusi.
Pia amewataka wananchi mbalimbali waweomba waendelee kujitokeza kutembelea maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa maarufu Sabasaba wanayoendelea kufanyika Dar es Salaam hususani kwenye bada la (Rita) ili waweze kupatiwa huduma mbalimbali ikiwemo vyeti vya kuzaliwa.
Kama kuna wananchi ambao wako karibu na Dar es Salaam, watumie nafasi hii ya kufika kwenye banda letu tumuhudumie na kwa wale ambao wapo mikoa ya mbali basi siyo mbaya nao wakatumia nafasi hii ya kutuma nyaraka zao mbalimbali kwenye tovuti yetu (Rita) wataweza kupata huduma zote za taasisi hiyo kwani Serikali yetu imejitahidi kuweka kila miundombinu mizuri ya kutoa huduma bora kwa wananchalisema Kanyusi.
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa