January 24, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rihanna

Rihanna awaomba msamaha Waislamu

NEW YORK, Marekani

MSANII wa muziki kutoka nchini Marekni, Robyn Rihanna Fent maarufu kama ‘Rihanna’, amewaomba msamaha waislamu kwa kutumia Hadith ya Kiislamu kwenye onesho la nguo za ndani za kampuni yake ya Fenty.

Rihanna mwenye umri wa miaka 32, alikosolewa vibaya mtandaoni kwa kutumia wimbo uaojulikana kama Doom wa msanii Coucou Chloe, ambao unajumuisha maudhui ya Kiislamu yanayofahamika kama Hadith.

Baadhi ya wafuasi wake wa Kiislamu walianza kuhoji matumizi ya wimbo huo kwenye onesho lake lilioneshwa moja kwa moja kupitia mtandao wa Amazon Oktoba 2 mwaka huu.

Akiomba msamaha huo kupitia kwenye ukurasa wake wa Instgram Rihana alisema, anajua amawakwaza sana Waislam hivyo anaomba msamaha kwani hakujua kama atawakwaza.

“Ningependa kuwashukuru jamii ya Waisilamu kwa kuonyesha uangalizi mkubwa ambao ulikuwa wa kukasirisha bila kukusudia katika onyesho letu kali la x fenty. Ningependa muhimu zaidi kuomba radhi kwa kosa hili la uaminifu, lakini la kupuuza.

“Tunaelewa kuwa tumewaumiza ndugu na dada zetu wengi wa Kiislamu, na nimevunjika moyo sana na hii! Sichezi na aina yoyote ya kutomheshimu Mungu au dini yoyote na kwa hivyo matumizi ya wimbo katika mradi wetu haukuwajibika kabisa!, tutahakikisha hakuna kitu kama hiki kitatokea tena. Asante kwa msamaha na uelewa, ” alisema Rihanna.

%%%%%%%%%