January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

RFB yaendelea kutoa elimu maonesho ya 8’8

Judith Ferdinand, Timesmajira Online

Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB), imeendelea kutoa elimu mbalimbali ikiwemo ya mfumo wa kieletroniki wa ufuatiliaji wa hali ya barabara kwa wananchi wanaotembelea banda lao katika maonesho ya kimataifa ya Nane Nane yanayofanyika jijini Mbeya.

Wananchi jijini Mbeya wakipata maelezo juu ya mfumo wa kielektroniki wa ufuatiliaji wa hali ya barabara unaowawezesha kutoa taarifa kwa haraka kupitia simu za kiganjani kutoka kwa Mhandisi Nedrick Godfrey wa Bodi ya Mfuko wa Barababara wakati waliotembelea banda la bodi hiyo lililopo katika maonesho ya kimataifa ya Nane Nane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini humo.

Akitoa elimu hiyo Mhandisi Nedrick Godfrey kutoka Bodi ya Mfuko wa Barababara,kwa wananchi waliotembelea katika banda lao amewaeleza juu ya mfumo wa kielektroniki wa ufuatiliaji wa hali ya barabara unaowawezesha wananchi kutoa taarifa kwa haraka kupitia simu za kiganjani kwa mamlaka husika kuhusu hali ya barabara ilivyo ili hatua za haraka zichukuliwe.

Hata hivyo uzinduzi wa mfumo wa kieletroniki wa ufuatiliaji wa hali ya barabara nchini ulifanyika jijini Mwanza,Julai mwaka 2022

Sanjari na hayo Mhandisi Nedrick ameeleza kuwa moja ya majukumu ya Bodi ya Mfuko wa Barabara ni pamoja na kukusanya fedha na kupeleka kwa wakala wa barabara nchini na baadae kufuatilia matumizi ya fedha hizo.

Madereva wa Bodaboda jijini Mbeya wakipata maelezo jinsi watumiaji wa vyombo vya moto wanavyochangia shilingi 263 ya matengezo ya barabara kutoka katika kila lita ya Petroli au Dizeli wanayonunua kutoka kwa Jastine Govela, Mtaalam wa Mifumo wa Bodi ya Mfuko wa Barababara wakati waliotembelea banda la bodi hiyo kwenye maonesho ya kimataifa ya Nane Nane yanayofanyika viwanja vya John Mwakangale jijini humo.

Kwa upande wake Mtaalam wa Mifumo kutoka Bodi ya Mfuko wa Barababara Jastine Govela,amewaelimisha wananchi na madereva bodaboda wa jijini Mbeya waliopata fursa ya kutembelea banda hilo juu ya umuhimu wa watumiaji wa vyombo vya moto katika matengenezo ya barabara na namna fedha inayopatikana kupitia watumiaji hao wa vyombo vya moto inavyotumika katika kukarabati miundombinu ya barabara nchini.

“Watumiaji wa vyombo vya moto mnachangia kiasi cha shilingi 263 ya matengenezo ya barabara kutoka katika kila lita ya petroli au dizeli mnayonunua kisha fedha hizo zinapelekwa katika kukarabati miundombinu hiyo ya barabara,”.

Ambapo mpaka sasa RFB imefanikiwa kuyafikia makundi mbalimbali ikiwemo wananchi na bodaboda kwa ajili ya kuwapa elimu hiyo.