Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM
KLABU ya Yanga imemtangaza MIGUEL ANGEL raia wa Argentina GAMONDI kuwa Kocha mpya wa klabu hiyo akichukua nafasi ya Nasriddine Nabi ambaye ameondoka baada ya msimu uliopita.
Miguel ana uzoefu na soka la Afrika kwa kufundisha Wydad Casablanca, Esperance de Tunis, Mamelodi Sundowns, ASEC Mimosas, USM Alger na Timu ya Taifa ya Burkina Faso.
Baadhi ya mafanikio yake akiwa Afrika ni kufika Nusu Fainali CAF Champions League msimu wa 2020|21 akiwa Kocha wa Wydady Casablanca
Msimu wa 2005|06 aliipa Mamelodi Sundowns ubingwa wa Ligi ya Afrika Kusini.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua