
Na Israel Mwaisaka, Rukwa
CHAMA Cha msalaba mwekundu (Red cross) wilayani Nkasi mkoani Rukwa kimefanya usafi kwa njia ya kujitolea kwenye chanzo Cha maji Mfili na katika ofisi ya mkuu wa Wilaya kama sehemu ya kukabiliana na athari za mvua ya El-Nino zinazoweza kujitokeza pindi mvua hizo zitakapoanza kunyesha.
Kazi hiyo imefanywa kwa kushirikiana na Wafanyakazi wa mamlaka ya maji mjini Namanyere ( NAUWASA) na jeshi la zima moto na uokozi walipoamua kuunga mkono jitihada hizo zilizoanzishwa na red Cross katika kufanya mji wa Namanyere kuwa safi ili kujikinga na maradhi ya kuambukiza yanayotokana na uchafu katika kipindi hilo Cha masika.

Akizungumzia mpango huo Mwenyekiti wa Red cross wa Wilaya Nkasi Israel Mwaisaka amesema kuwa wao kama taasisi ya kujitolea katika kukabiliana na majanga mbalimbali wameona kwamba Kinga ni bora kuliko tiba ndiyo maana wameanza na suala zima la usafi kama hatua za awali za kuzuia majanga yasiweze kutokea.
Amesema kuwa kitendo cha jeshi la zima moto na uokozi na Wafanyakazi wa NAUWASA kuunga jitihada hizo imewatia moyo na nguvu ya kuendelea na kazi hizo za kujitolea na lengo lao kuu ni kutaka kuona mvua za El-Nino hazileti madhara kwa jamii hasa ya maradhi yanayotokana na uchafu ambao wanaweza wakauzuia
Amefafanua kuwa kwa sasa wao kama Red cross wameyaainisha maeneo yote ya Umma yenye uchafu ambayo watakwenda kuyafanyia usafi na wangeomba Wananchi wa maeneo ambayo watakuwepo kwa usafi na wao wawe wanajitokeza kuungana nao kufanya usafi.
Baadhi ya Wananchi walioungana na Red Cross kufanya usafi huo wamedai kuwa uamuzi wa Red cross kujitoa kufanya usafi ni jambo kubwa ambalo wanatakiwa kuungwa mkono.

Jellad Silivesta mmoja wa Wananchi waliojitokeza alisema kwamba yeye binafsi amefurahishwa na jinsi usafi ulivyofanyika kwenye chanzo Cha maji cha Mfili kwani wao wanakitegemea sana chanzo hicho cha maji na kuwa hakuwa na sababu ya kutoshiriki katika kazi hiyo na kuwaomba Watu wengine kuwaunga mkono Red cross katika jitihada hizo walizozianzisha
Kaimu Katibu tawala wa Wilaya Nkasi ambaye pia ni afisa tawala Alpha Noah amefurahishwa na moyo waliouonyesha Red Cross wa kuamua kujitoa kwa kujitolea kufanya usafi katika maeneo ya Umma na kuwa wao kama Serikali wapo tayari kushirikiana nao katika kuona mipango yao hiyo inafanikiwa na kubwa ni jamii kunufaika programme hizo



More Stories
Uchaguzi wa TUCTA wasitishwa na Mahakama Kuu
Kalimbaga ataja vipaumbele vitano ARMFA
Dkt.Gwajima azindua chuo cha wasichana