Na Mwandishi wetu,timesmajira,online
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam,Amos Makalla amewataka Wananchi kuchukuwa tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Corona huku amepiga marufuku Wananchi kuingia kwenye vyombo vya usafiri na sehemu za kutoa huduma pasipo kuvaa barakoa.
RC Makalla ametoa maelekezo hayo Kufuatia Mwongozo uliotolewa na Wizara ya Afya hivi karibuni wakati akiongea na waandishi wa habari.
Makalla amesema anatarajia kuanza kufanya ziara za kustukiza kwenye Vituo vya Daladala, Feri, Stendi ya Mabasi ya Mwendokasi, maeneo ya Masoko na sehemu zote za kutoa huduma ili kuangalia Utekelezaji wa agizo hilo kama linafanyika.
Aidha RC Makalla amesema Serikali imejipanga kutoa huduma Bora za matibabu kwa wagonjwa wote watakaofika hospital na kuwataka Wananchi watakaoona dalili za Corona kuwahi vituo vya Afya.
More Stories
Rais Samia aomboleza kifo cha Papa Francisko
Papa Francis afariki Jumatatu ya Pasaka akiwa na miaka 88
Kanisa la Shincheonji la Yesu nchini Ufaransa lakanusha ripoti ya Le Parisie