Na Israel Mwaisaka, TimesMajira Online, Rukwa
MKUU wa Mkoa Rukwa Charles Makongoro Nyerere amewataka Watendaji wa halmashauri ya wilaya Nkasi kuhakikisha wanajipanga vizuri na kujibu hoja zote ili ziweze kufungwa.
Agizo hilo amelitoa kwenye baraza maalumu la Madiwani la hoja ambapo amedai kuwa kumekuwepo na hoja nyingi ambazo zimezalishwa kizembe kwa sababu ya kukosekana kwa majibu na kutolewa kwa wakati.
Alisema kuwa halmashauri ya wilaya Nkasi imeonekana kuwa na hoja nyingi sana za ukaguzi na kuwa hoja nyingi zinajibiwa na kama majibu yangepatikana kwa wakati baadhi ya hoja zisingekuwepo.
Pia mkuu huyo wa mkoa alimtaka mkurugenzi mtendaji wa wilaya kufuatilia kwa kina utendaji wa wafanyakazi wa idara ya manunuzi kwani ukifuatilia wao ndiyo wamekuwa wazalishaji wa hoja nyingi kiasi kwamba kama wangekuwa makini uenda hoja zingekuwa chache na kujibika.
Hivyo aliwataka Watumishi wote wa halmashauri ya wilaya Nkasi kuwa wamoja kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuhakikisha hoja zote zinajibiwa tena kwa wakati na kuwa kama watajenga utamaduni wa kufanya kazi kwa umoja na upendo uenda katika awamu ijayo hoja zikapungua kwa kiasi kikubwa au zikatoweka kabisaHalmashauri ya wilaya Nkasi katika kipindi cha mwaka 2021/2023 ilipata hati ya mashaka na kuiagiza taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) kuhakikisha wanaifuatilia miradi yote inayotekelezwa ndani ya wilaya na kuhakikisha wanampatia taarifa katika kipindi kifupi.
Katibu tawala wa mkoa Gerald Kusaya kwa upande wake alitaka kila mmoja ambaye amesababisha hoja katika eneo lake awajibishwe ili kuonas kwamba katika kipindi kingine kijacho asiweze kufanya uzembe unaoweza kupelekea kupata hati yenye mashaka au chafu na lengo la mkoa ni kutaka kuona halmashauri zote za mkoa Rukwa zinapata hati safi.
Na aliwataka Madiwani kuwa mstari wa mbele katika kusimamia shughuli za maendeleo kwa kushirikiana na Watendaji wa serikali katika maeneo yao na kuwa kufanya hivyo kutachagiza maendeleo na hakuna miradi itakayokwama na kutokuwepo kwa hoja nyingi za ukazi.
Awali mtunza hazina wa halmashauri CPA Erick Kilimo alieleza kuwa kupatikana kwa hati ya mashaka kulisababibishwa na uwasilishwaji hafifu wa viambata na kuwa kama viata hivyo vingewasilishwa kwa wakati huenda upatikanaji wa hati ya mashaka usingekuwepo.
Mkaguzi mkuu wa nje Baraka Mfugale aliainisha baadhi ya mambo ambayo yamepelekea kupatikana kwa hati yenye mashaka na kuwa kama watayazingatia wataweza kufuta hoja zote na kuwa katika kipindi kijacho hawataweza kuwa na hoja.
Madiwani kwa upande wao walidai kuwa ipo haja ya kuwashughulikia watendaji ambao wamezalisha hoja na kuwa lengo lao ni kutaka kuona halmashauri yao ipo salama na maendeleo yanawafikia wananchi wao.
More Stories
Mwanasiasa mkongwe afariki Dunia
Rais Samia Kuzindua Sera Mpya ya Elimu na Mafunzo
Jokate awapa tano vijana UVCCM maandalizi Mkutano Mkuu wa CCM