Na Raphael Okello,Timesmajira Online,Musoma.
MKUU wa Mkoa wa Mara, Said Mtanda amewataka watendaji wakuu katika Halmashauri za Wilaya ya Musoma na Bunda kuhamia katika majengo ya ofisi zao mpya ifikapo Oktoba 20 mwaka huu .
Mtanda ametoa agizo hilo septemba 27 wakati alipokuwa kwenye ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa hospitali ,vituo vya afya pamoja na shule mpya za sekondari katika Halmashauri ya Musoma.
Amekumbusha kuwa ujenzi wa majengo ya ulianza tangu 2021 lakini hadi sasa halmashauri hizo zimeshindwa kuhamia katika ofisi hizo ili kuwahudumia wananchi kwa karibu.
“Nawaagiza ifikapo Oktoba 20, mwaka huu msipohamia katika majengo ya ofisi zenu za halmashauri nitawatumia JKT kuhamisha vifaa vyote na kuvileta katika majengo haya,hivyo vivyo ujumbe huu uwafikie Halmashauri ya Wilaya ya Bunda,”amesema Mtanda.
Akiwa katika ukaguzi wa miradi hiyo katika Halmashauri ya Musoma aliwapongeza viongozi wa halmashauri hizo kusimamia vizuri manunuzi ya vifaa vya ujenzi wa miradi na kushirikiana vizuri na wananchi katika ujenzi wa miradi.
Amewaomba viongozi wa CCM katika wilaya za Mkoa wa Mara kuendelea kusimamia kikamilifu bila kuona aibu utekelezaji wa miradi mbalimbali kama ilani ya CCM inavyosema.
Mtanda alipokea pia taarifa ya ujenzi wa vituo vya afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma na kuhimiza utoaji bora za huduma za afya katika halmashauri hiyo.
Akitoa taarifa ya ujenzi wa kituo cha afya cha Kiriba, Mtendaji wa kata ya kiriba, Victor Edward amesema wamepokea jumla ya shilingi Milioni 750 .
Amefafanua kuwa awamu ya kwanza walipokea milioni 500 na awamu ya pili kiasi cha shilingi milioni 250.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba