January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

RC Mgumba aipongeza GBP kwa uwekezaji

Na Hadija Bagasha, TimesMajira Online, Tanga

Mkuu wa mkoa wa Tanga Omari Mgumba ameipongeza kampuni ya mafuta ya GBP kwa uwekezaji mkubwa inayoendelea kuufanya ambapo kwa kiasi kikubwa imekuwa na mchango mkubwa kwa Maendeleo ya mkoa na kuchangia pato la taifa.

Mgumba alitoa pongezi hizo ikiwa ni mara ya kwanza ya ziara zake kutembelea na kujionea miradi mbalimbali Mkoani Tanga ambapo alisema kuwa adhima ya serikali ni kufungua uchumi pamoja na kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji ambao wamekuwa ni wadau wakubwa wa maendeleo.

Mgumba alisema kuwa Tanga ambayo Sasa imekuwa ni kivutio kikubwa kwa wawekezaji kutokana na ujio wa Bomba la mafuta wamejipanga kuhakikisha kuwa wanaendelea kuweka mazingira rafiki pamoja na kuondoka vikwazo kwa wafanyabiashara wa mafuta hapa nchini kuitumia bandari ya Tanga.

“Niwapongeze sana kwa kazi nzuri mnayoifanya na sisi serikali inafarijika na uwepo wenu mna mchango mkubwa kwenye taifa hili kiuchumi pamoja na kutoa ajira kwa watanzania na mimi kwakuona hilo ninawatakia kila la kheri” alisema Mgumba.

Mara baada ya Mkuu wa Mkoa kutembelea bohari ya mafuta ya GBP uongozi wa bohari hiyo umemuomba kuingilia kati viwango vya bei vya EWURA ambavyo vinasababisha wafanyabiashara wa mafuta kanda ya kaskazini kuchukulia bidhaa hiyo bandari ya Dar es Salaam badala ya bandari ya Tanga.

Akizungumza meneja meneja usimamizi wa GBP, Fahimu Salimu alisema kuwa wanaendelea kuboresha miundombinu katika bohari yao ili kuwawezesha kutoa huduma kwa wafanyabiashara wa mafuta hapa nchini huku wakiwa wanatoa magari 80 ya mafuta kwa siku.

Aidha amezitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili ambapo alisema kuwa kuchelewa kwa meli ya mafuta kuja hapa nchini inapelekea kushindwa kutoa huduma hiyo kwa ufanisi.

“GBP ni moja ya kituo kikubwa cha mafuta na uwezo wake ni mkubwa tulibadilisha miundombinu yetu ya mabomba Mara nyingi meli ukichelewa inakuwa ni changamoto na hasara kwetu sisi” alisema