January 15, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

RC Mbeya awataka wakala wa barabara kuharakisha ujenzi 

Na Esther Macha, Timesmajira,Online,Mbeya 

KUFUATIA ajali iliyoua watu watano Mkuu  wa Mkoa wa Mbeya ,Juma Homera ameagiza wakala wa barabara mkoani hapa (Tanroad)kuharakisha kujenga miundombinu ya kusimama magari makubwa ya  mizigo yanayotoka nchi jirani za Zambia,Malawi na Congo na kuwepo kwa utaratibu wa kupishana kw magari kwa zamu  yanayokwenda Mbeya mjini na njia kuu ya Jijini  Dar  Es Salaam.

 Hayo yamesemwa leo  wakati akizungumza na waandishi wa habari kufuatia  ajali mbaya ya Lori la lililobeba shehena ya Mahindi  na kugonga basi la abiria aina ya Costa na kusababisha vifo vya watu watano papo hapo.

Aidha Homera amesema  kuwa wakati Serikali ya awamu ya Sita ikiendelea na utekelezaji wa mradi mkubwa wa bararabara za mchepuo za njia nne kutoka Uyole mpaka Igawa  kwa sasa Tanroad waanze kujenga vituo vya muda vya kupumzikia magari makubwa na madogo.

Hata hivyo Homera amsema kuwa eneo hilo limekuwa lilitokea ajali za mara kwa mara huku akibainisha hiyo ni tatu kutokea  kwa nyakati tofauti ndani ya mwezi June ya Julai Mwaka huu.

Kwa  upande wake Mkurugenzi wa Hosptali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya (MZRH) Dkt. ,Godlove Mbwanji amesema kuwa katika ajali ya jana walipokea majeruhi  saba kati ya hao wanawake watano na wanaume wawili ambao ni Neema Gaitan (33) mkazi wa Mbarali ,Atu Tukae (32) mkaz wa Uyole ,Grace  Konzo (42) mkazi Sinde ,Eva Kajengaje((35)mkazi wa Mbarali ,Jane Mwasebile (49),kazi wa Rungwe na omary kihanga .

Hata hivyo Dkt,Mbwanji amesema kuwa majeruhi hao wanaendelea vizuri ambapo kati ya hao mmoja ameruhusiwa huku wangine wakiendelea na matibabu .

Awali taarifa za Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ,Urlich Matei amesema kuwa majeruhi wa ajali hiyo wamelazwa kwenye kituo cha Afya Inyala na Hosptali ya Wilaya Igawilo na kwamba atatoa taarifa ya majina ya majeruhi wa walipoteza maisha .