December 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

RC Makonda atoa miezi 3 kwa Kamishna wa Ardhi Arusha

Atangaza ujio wa ziara ya Mikutano ya hadhara kuzungumza na kusikiliza kero za Wananchi wa Arusha

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda amemtaka Kamishina wa Ardhi mkoa huo kushughulikia ipasavyo suala la migogoro ya ardhi kuhakikisha inakwisha.

Makonda ameyasema hayo leo tarehe 8 Aprili , 2024 wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza kwa wingi nje ya Ofisi yake.

Akizungumza na Wananchi, Makonda amepokea malalamiko ya migogoro ya ardhi na kutoa miezi 3 kwa Kamishina wa Ardhi ambapo amemueleza kuwa kama iwapo hatotekeleza wajibu wake ipasavyo basi ajiandae kuandika barua ya kuachia nafasi hiyo.