December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

RC Makalla:Maonesho ya 46 ya Sabasaba yamefana

Na Penina Malundo,timesmajira, Online

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla amesema Sera nzuri na mwelekeo Bora alioonyesha Rais Samia Suluhu Hassan kuitangaza Nchi kimataifa hususani Royal tour vimechagiza Maonesho ya 46 ya sabasaba kuwa na mwamko mkubwa na ushiriki wa Makampuni mengi kutoka ndani na nje ya Nchi.

RC Makalla amesema hayo leo alipotembelea Maonyesho hayo ambapo amefurahi kuona zaidi ya Nchi 22 zikishiriki Maonyesho hayo na Kampuni za 3,200 za Ndani 180 kutoka nje ya Nchi.

Aidha RC Makalla ameipongeza Tantrade kwa kuratibu vizuri Maonesho hayo na kutoa wito kwa Wananchi kutembelea Maonesho hayo ili kujionea ubunifu na bidhaa mbalimbali.

Pamoja na hayo RC Makalla amepongeza pia ubunifu wa kuanzisha route za Usafiri wa Mabasi ya mwendokasi mpaka kwenye Viwanja hivyo jambo linalorahisisha huduma ya usafiri kwa wananchi wanaoenda kutembelea Maonesho hayo.