December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

RC Makalla aagiza uongozi wa Jiji kuwapatia walemavu eneo la karume kufanyia biashara

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Ilala na Mkurugenzi wa Jiji la Ilala kushirikiana Na Uongozi wa Chama Cha walemavu mkoa wa Dar es salaam kuwapatia eneo la Karume kufanya biashara zao baada ya kupisha eneo la Njia Za wapita kwa miguu.

Mkuu wa Mkoa akiongea Na walemavu hao aliwaambia kuwa kila alipofanya mazungumzo Na mkuu wa Wilaya alimuhakikishia kuwa suala la walemavu alikuwa analishughulikia vizuri Na bahati mbaya kabla hawajafikia muafaka baadhi ya meza zilipotea usiku wa kuamkia jana
Kufuatia tukio hilo Mkuu wa Mkoa alikubali ombi la walemavu Hao kupatiwa eneo lingine la biashara japokuwa chama Cha walemavu wamepewa vibanda 300 machinga complex Na vibanda vingine eneo la karume.

Kuhusu ombi la walemavu kuomba Mkuu wa mkoa kutengua uamuzi wake wa kuruhusu bodaboda kuingia mjini, Mkuu wa mkoa aliwaeleza kuwa ameunda kamati Na ameipa kamati miezi 3 ili kuanisha vituo vya Bodaboda Na aliwasihi wawe watulivu Na wawe tayari kufanya kazi kwa pamoja Na bodaboda katika mpango utakaokuwa umeratibiwa vizuri.