December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rc.Makala aipongeza Ilemela kuendelea kupata hati safi kwa kipindi cha miaka mitatu

Judith Ferdinand, Timesmajira online, Mwanza

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza CPA.Amos Makalla ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kwa kupata hati safi katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022, ikiwa ni mara tatu mfululizo kuanzia mwaka wa fedha 2019/2020, 2020/2021 na 2021/2022.

amezitoa pongezi hizo katika Mkutano maalum wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kwa ajili ya kujadili utekelezaji wa hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG)

Pia amesema kuwa wananchi wanafuatilia sana utendaji wa Halmashauri pamoja na taarifa mbalimbali, hivyo kuwa na hati safi kunawajengea imani.

Hata hivyo amewataka Madiwani wa halmashauri hiyo kusimamia kidete maslahi mapana ya wananchi kwa kufanyia kazi taarifa ya Mkaguzi wa ndani kila anapoiwasilisha ili kusaidia kupunguza hoja.

“Ushauri wangu ili kuendelea kupunguza hoja ambazo sio za lazima Menejimenti ishirikane na CAG katika hatua zote za ukaguzi naamini hoja zitapungua,”amesema Makalla.

Diwani wa Kata ya Pasiansi Rose Mayunga ametoa ushauri kwa wataalam kuhakikisha wanatunza vielelezo vyote ili kuepusha hoja na mwisho wa siku Ilemela iwe na hoja ambazo zinafungwa

Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Manusura Lusigaliye ameahidi kuwa Baraza la Madiwani kwa kushirikiana na watalaam watafanyia kazi maelekezo yote ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa hoja zilizobakia zinafungwa.