Na Yusuph Mussa,Timesmajira Online,Pangani
MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anafanya kazi kubwa ya kuboresha miundombinu ikiwemo ya maji na kuhakikisha wananchi wanapata maji, na kuwatua ndoo kichwani wanawake nchini.
Ameyasema hayo Oktoba 19, 2023 wakati akiweka Jiwe la Msingi kwenye mradi wa Maji Tungamaa uliopo Kijiji cha Tungamaa, Kata ya Tungamaa, Wilaya ya Pangani mkoani Tanga.
“Kazi zinazofanywa na Rais Samia ameigusa sekta muhimu ya maji kila kitu kinahitaji maji, usipoyanywa, utaoga, ama kunawa,sisi watu wa Pwani ametufanyia jambo kubwa hapa Pangani, na maeneo mengine ya nchi,wananchi tuendelee kumuunga mkono,”amesema.
Kindamba amesema mradi huo umefika asilimia 72 huku matarajio ni kukamilika Novemba mwishoni, mwaka huu ambapo tenki linauwezo wa ni lita 50,000, mahitaji lita 61,000 kwa siku, na kisima kina uwezo wa kuzalisha maji lita 5,000 kwa saa, hivyo upatikanaji wa maji utazidi mahitaji ya wananchi” amesema Kindamba.
Kindamba amesema Rais Dkt. Samia anamwaga fedha nyingi kwenye miradi mbalimbali katika huduma za jamii, kwani amekuwa akitoa fedha kwenye sekta zote.
“Rais Dkt. Samia anamwaga fedha nyingi kwenye miradi mbalimbali katika huduma za jamii, kwani amekuwa akitoa fedha kwenye sekta zote,kwenye maji utamkuta, afya utamkuta, barabara utamkuta, na kwenye nishati utamkuta, hivyo hilo ni jambo la kutukuka,” amesema Kindamba.
Kindamba amesema fedha zinazotolewa ni nyingi, hivyo wananchi wanatakiwa kulinda miundombinu ya maji, hivyo wasikubali watu kwenda kuvuruga ama kuharibu miundombinu hiyo.
Meneja wa Wakala wa Majisafi na Uaafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo amesema nia na mipango yao ni kutekeleza Ilani ya CCM 2020- 2025, wanataka kuona wananchi wa vijijini wanapata maji kwa asilimia 85 ifikapo mwaka 2025.
Meneja wa RUWASA Wilaya ya Pangani Mhandisi Rajabu Yahya amesema mradi huo unajengwa kwa thamani ya sh. milioni 513, na wanufaika wa mradi ni wananchi 2,047, vituo vya maji (vilula) 13, urefu wa mtandao wa bomba mita 5,234, tenki likiwa na ujazo wa lita 50,000 katika mnara wa mita tisa, uwezo wa kisima ni kuzalisha lita 5,000 kwa saa.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa