November 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

RC Dar apiga marufuku michango shuleni

Na Heri Shaaban,TimesMajira Online,Dar

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala amepiga marufuku michango ya Shuleni bila kibali cha Serikali pamoja na ‘Tution’.

Mkuu wa mkoa Makala ameyasema hayo katika ziara yake Jimbo la Segerea Wilaya ya Ilala ya kutatua kero za wananchi .

“Ninaagiza katika mkoa wangu wa Dar es Salaam marufuku michango na tuisheni shuleni bila kibali tutekeleze mpango wa elimu bila malipo bila kuwachanja wananchi fedha amesema Makala.

Makala amesema Waraka wa Serikali Elimu bila malipo hivyo walimu wasiwachangishe pesa za tuisheni Wazazi.

Katika hatua nyingine amepiga marufuku ujenzi holela wa vibanda vya viabashara katika maeneo ya shuleni mkoa wa Dar es Salaam bila kufuata taratibu

Makala amesema kuna baadhi ya shule zimejenga vibanda bila kufuata taratibu katika mkoa wake ni marufuku kuanzia Leo .

Wakati huo huo ameagiza DAWASA kuweka kambi Buguruni kwa ajili ya kuzibua mfumo wa maji taka ambao unachafua mazingira ya wakazi wa Buguruni kila wakati.

“Ninaagiza DAWASA kuweka kambi Kata ya Buguruni kutengeneza miundombinu ya maji taka ambayo ni ya muda mrefu imekuwa kero kwa jamii” amesema.

Katika ziara hiyo mkuu wa mkoa anatembea na wakuu wa Idara wote na Wataalam wake ,baadhi ya mashauri yanatatuliwa hapo hapo mengine anayaekeleza mahala mamlaka husika .

Kwa upande wake Mhandisi wa DAWASA mkoa wa Kinyerezi Burton Mwalupaso alisema DAWASA jukumu lao kuakikisha linasambaza maji safi na Salama kwa wananchi pia jukumu lao lingine kusimamia maji taka agizo lililotolewa na Mkuu wa mkoa watatekeleza na kutatua kero hiyo.