November 14, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

RC Chalamila azuia bomoabomoa Mbagala Msongola

Na Heri Shaaban , TimesMajira Online

MKUU wa Mkoa Dar es Salaam Albert John Chalamila , amesitisha Bomoabomoa katika wilaya TEMEKE Mbagala kuelekea Msongola ,katika nyumba za wananchi na vibanda vya Biashara walipoweka alama ya X wakala wa Barabara Tanzania TANRODS mkoa Dar es Salaam.

“Nina agiza wakala wa Barabara TANRODS marufuku kubomoa nyumba zote zilizowekwa alama ya X na vibanda vya biashara mpaka hapo nitakapotoa tamko kwa kujilidhisha na kufanyia kazi maelezo ya Mbunge wa Mbagala Abdalah Chaurembo anayejua historia ya Barabara ya Mbagala ,Mbande kuelekea Msongola “alisema Chalamila.

Mkuu wa mkoa Albert Chalamila, alisema katika suala la Bomoabomoa kuna kucheka na kulia aliagiza TANRODS wajilidhishe wakishindwa waache wasibomoe Maelezo ya historia ya Barabara hiyo Mbagala kuelekea Mbande mpaka Msongola Mbunge Abdalah Chaurembo ameeleza vizuri .

Aliwataka Wananchi wa Jimbo la Mbagala wasifanye kazi na Mbunge asiyewajibika kutumikia wananchi badala yake wafanye kazi na Mbunge wao Chaurembo ambaye anatatua kero za wananchi na kushirikiana nao.

Mbunge wa Jimbo la Mbagala Abdalah Chaurembo alisema Bomoabomoa hiyo imeanzia Msongola,Mbande, kuelekea Mbagala wananchi wake waliwekewa alama ya X ambapo aliwataka wananchi wake wasiandamane wala kuchanga pesa kutafuta Mwanasheria badala yake amewataka wakae wafuate taratibu.

MBUNGE Chaurembo alisema kila Barabara taratibu zote zinafamika kila upande wa Barabara kuacha mita 30 ambapo alisema miaka ya nyuma maeneo hayo yalikuwa mashamba ya kijiji baadae kujenga makazi.

Aidha alisema wamekuwa wakiishi hivyo ambapo mpaka leo ukitaka kukata mnazi lazima uzungumze na Mwenyewe mwaka 1978 wale waliozaliwa mji huo Jando la unyago wanafanyiwa eneo hilo la Chamazi na Mkole pia walikuwa wanafanyia hapo hapo.

“Mwaka 1977 wazee walifeka Barabara ili mabasi yaweze kufika wakati huo ADUKO walikuwa wakichukua mita 15 kulia na kushoto mwaka 2018 Wakala wa Barabara Tanzania TANRODS waliweka mawe makubwa wakisema sheria ya mwaka 1932 inasema hivyo alama ya X ya Bluu eneo la Serikali na alama nyekundu wananchi watalipwa lakini wafanyakazi wa TANRODS wa sasa hivi ni wapya. Wameanza kazi mwaka 2017 hawafahamu historia ya Barabara Mbagala, Chamazi ,Mpaka Msongola”alisema Chaurembo.

Mbunge Chaurembo ameagiza TANRODS kuleta uthibitisho wa mwaka 1932 wakishindwa kuleta uthibitisho huo hawafai kufanya kazi TANRODS.

Mhandisi wa Barabara Mkoa Dar es Salaam ENG JOHN MKUMBO alisema ni kweli Ofisi yake imeweka alama ya Bomoabomoa X ambapo wapo waliopewa wito wa kubomoa siku 14 na siku 30 na February ndio ilikuwa mwisho nyumba zote ziwe zimebomolewa lakini kwa sasa zoezi hilo tumesimamisha mpaka hapo watakapojilidhisha.