January 27, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rc Chalamila azitaka halmashauri za Mkoa kufanya kazi kwa ukaribu na Ofisi CAG

Na Mwandishi wetu,Timesmajira, Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Juni 26,2024 akiwa katika muendelezo wa kushiriki mabaraza ya Hoja za Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali CAG kwa nyakati tofauti katika Manispaa ya Ubungo na Kinondoni amezitaka Halmashauri hizo kufanya kazi kwa karibu na ofisi ya CAG ili kuondokana na hoja zisizo za lazima

RC Chalamila amesema wakurugenzi wa Halmashauri na ofisi ya CAG wasikimbiane ni vema kufanya kazi kwa karibu ili kuondokana na hoja zisizo za lazima pia kuzingatia ushauri unaotolewa na wakaguzi wa ndani.

Aidha RC Chalamila amewataka wakuu wa Idara na vitengo kutoa ushirikiano kwa karibu wakati timu ya GAG inapotekeleza majukumu yake katika Halmashauri husika.

Kwa upande wa Katibu Tawala wa Mkoa Dkt Toba Nguvila akiongea wakati anamkaribisha Mkuu wa Mkoa amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kuendelea kusimamia maagizo yake ambapo amezitaka Halmashauri kujikita katika umahiri wa kuzuia hoja za CAG na Sio umahiri wa kujibu hoja

Sanjari na hilo RC Chalamila amezitaka Halmashauri kusimamia vema ukusanyaji wa mapato na kubuni vyanzo vingine vipya pia kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato pamoja na hilo ameipongeza Manispaa ya Ubungo kwa kupata Hati safi miaka mitano mfululizo na Manispaa ya Kinondoni kwa kupata Hati safi miaka mitatu mfululizo