January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, akizungumza kwenye mkutano wa viongozi wa dini

RC Chalamila awataka viongozi kuendelea kuombea Uchaguzi Mkuu

RC Chalamila awataka viongozi
kuendelea kuombea Uchaguzi Mkuu

Na Esther Macha,TimesMajira,Online , Mbeya

MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amesema Taifa litakuwa katika mikono salama endapo viongozi wa dini wataendelea kusimama imara kuombea mchakato wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28, mwaka huu.

Aidha amewasihi waendelee na maombi ili Taifa liweze kupata kiongozi sahihi atakayeendelea kuhakikisha Tanzania inaendelea kubaki kwa kuwa nchi yenye utulivu na amani yenye kupiga hatua za kimaendeleo kwa kasi kubwa.

Mkuu huyo wa mkoa amesema hayo jana wakati akizungumza na viongozi wa dini kuhusu ,amani na utulivu kuelekea uchaguzi mkuu na maendeleo katika Mkoa wa Mbeya.

Aidha, Chalamila amesena madhara ya kupata kiongozi asiye sahihi aliyeingia bila ya hofu ya Mungu ni kusimama upande wa shetani .

“Ndugu zangu kama hamtapata kiongozi mwenye nguvu ya kukemea basi tujue viongozi wa dini kuna sehemu mlilegea katika majukumu yenu ya kusaidia Taifa,”amesema Chalamila .

Amesema misimamo na maonyo ya kikanisa ni muhimu sana na wakiwaacha viongozi wakizagaa kama kondoo ambao hawana wachungaji wake( viongozi wa dini) katika taifa watakuwa wamewaonea kwa sababu hata wakiwa watoto wadogo huonywa .

Kwa upande wake kiongozi wa Kanisa Halisi la Mungu, Baba (UWAMBENE) Kuhan Shangwe amesema waumini wana akili sana wanajua kupambanua vizuri mambo na kuahidi kuwa wataendelea kuliombea taifa .

Viongozi wa dini wakiwa kwenye mkutano huo

Kwa upande wake Shekhe Mkoa wa Mbeya,Mohamed Mwansansu amesema Rais Magufuli lazima aheshimiwe kwani kudharau mamlaka ya nchi ni kuhatarisha amani ya nchi .

“Vitu alivyovifanya Rais Magufuli vinaonekana wazi leo hii unaingia kwenye malumbano ya kutotambua kazi alizofanya hii haipendezi ,hebu tumuunge mkono Rais Magufuli ili aweze kutekeleza miradi ya maendeleo,” amesema.