Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amesema ameona taarifa kuhusu baadhi ya Watu kuwa na dhamira ya kuandamana Jijini Dar es salaam leo wakidai kupinga kilichoamuliwa kuhusu ubia wa uendelezaji wa Bandari kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai ambapo amewataka waliokusudia kuandamana waache mara moja kwa kile alichosema kuwa huu sio muda wa maandamano.
“Ndugu Waandishi wa Habari tumeitana leo Jumatatu ili tuweze kuzungumza baadhi ya mambo ambayo nimeona yameanza kupigiwa kelele kupitia mitandaoni na kupitia kwenye makundi ambao hawalitakii mema Taifa letu”
“Nimeona baadhi ya Watu kuwa na adhima ya kuandamana wakidai wanapinga kilichoamuliwa kuhusu ubia wa uendelezaji wa Bandari kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai, kuna Kijana mmoja amepeleka barua kuonesha yeye anataka kufanya jukumu hilo”
“Kwa ujumla tumeelekeza huu sio muda wa maandamano hata kidogo, jambo hili kwa Mtu anayetaka kulifahamu kuna njia sahihi la kulifahamu, maandamano yanasitisha muda wa biashara na Watu kupata huduma za haraka za Hospitali, kwa mantiki hiyo Vijana wote ambao wamekusudia kufanya haya basi waache mara moja”
Maandamano hayo ya amani yameitishwa na Kijana Mwanaharakati wa Haki za Binadamu Deusdedith Soka ambapo amenukuliwa akisema lengo la maandamano hayo yaliyopangwa kufanyika leo kuelekea Ikulu ya Magogoni ni kupinga mkataba wa Bandari kati ya Serikali ya Tanzania na DP World.
More Stories
Jokate awapa tano vijana UVCCM maandalizi Mkutano Mkuu wa CCM
Watakaokwamisha mapato Kaliua kukiona cha moto
Dkt.Gwajima aagiza kuundwa kamati za ulinzi wa watoto