Akagua miundombinu ya barabara, maeneo yaliyotuama maji na mabonde ya mito mbalimbali aliyoathiriwa nyakati za mvua.
Na Penina Malundo, Timesmajira
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Albert Chalamila akiwa na timu ya wataalam amekagua maeneo mbalimbali Katika Mkoa huo ambayo yaliathiriwa kwa kiasi kikubwa na mvua kwa kutumia ndege maalum ya TANAPA.
RC Chalamila akiongea na waandishi wa habari Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl JK Nyerere Terminal I kabla ya kuruka na ndege hiyo, amesema mvua zilizonyesha katika mkoa huo zimeleta athari kubwa hivyo ameona ni vema kukagua kujionea hali halisi ya athari ya mvua hiyo ilivyonyesha .
Amesema baada ya ziara hiyo atakuja na suluhu ya pamoja ya kuona namna maboresho wanayotakiwa kuyafanya kwani tayari Rais Samia Suluhu Hassan ametenga fedha kwaajili ya kufanya uboreshaji ya maeneo yaliyoathiriwa.
Katika ziara hiyo ,RC Chalamila ameambatana na wataalam wa Ardhi, Kamati ya usalama, Mganga Mkuu wa Mkoa, Wataalam wa bonde pamoja na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam.
Katika ukaguzi wake RC Chalamila amesema watakagua athari za mvua katika mabonde ya mito mbalimbali ikiwemo Msimbazi, Nyakasangwe, Mpigi na mto Mzinga, vilevile maeneo ambayo yamejengwa holela, pia maeneo ambayo maji yametuama ili yasisababishe magonjwa, na barabara ambazo zilipata athari za mvua ili badaye kuja na namna bora ya kurejesha miundombinu hiyo.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba