January 26, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ray Vanny ampa makavu Harmonize

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MSANII wa muziki wa Bongo fleva kutoka WCB ambaye kwa sasa bosi wa Next Level Music, Ray Vanny amempa makavu msanii mwenzake na Bosi wa Kondegang Rajabu Abdul maarufu kama ‘Harmonize’ kwa kitendo cha kutaka kutembea na mtoto wa aliyekuwa mpenzi wake Kajala Masanja, ajulikanae kwa jina la Paula.

Akitoa makavu hayo kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram Ray Vanny amesema, Dunia inamaajabu yake lakini hajawahi kuona mtu wa ajabu kama Harmonize ambae anataka kua na mama na mtoto, tena kwa nguvu zote na kutuma hadi utupu wake bila hata kuogopa nafasi ulionayo kwenye jamii.

“Harmonize ni mtu wa Ajabu sana umejidhalilisha sana kua kama ulivyozaliwa na angali wewe ni kioo cha jamii. Ni roho ya ajabu sana ulionayo yani kila nikikuwaza sipati jibu ndugu yangu. Ulikua unawapigia simu viongozi mbalimbali juu ya swala langu mimi sasa nawaza leo hii utawaangaliaje ?? Wewe ni balozi wa kampuni na zimekupa heshima kama balozi, sasa nawaza unapata wapi ujasiri wa kutuma utupu wako ni kampuni gani inakubali fedheha hii na je wanakuonaje kwa kitendo hiki ulichokifanya kinachodhalilisha wanawake hasa mama?.

“Hivi hukumfikiria mama ambae aliekupa heshima wewe na kukuweka karibu na kukutambulisha familia yake?. Yani unataka ukatembee na mwanae wa damu yani mwanae wakumzaa?, leo hii mwanao wa kike akikua akasikia uchafu huu anakuona ni baba wa namna gani wewe unaemtaka Mama na Mtoto.

“Ushauri wangu. Omba radhi kwa wazazi na kina Mama, nikiwa na maana wanawake ambao ni Mama zetu wanastahili heshima sio kudhalilishwa kama ulivyofanya wewe na unaigiza kama hakijatokea kitu. Hukiheshimiwa basi jiheshimu,” amesema Rayvanny.

%%%%%%%%%%%%%%%%