November 7, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rastafari yaiomba serikali kurudisha jamii katika uhalisia wa mwafrika

Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza

Jamii ya imani ya Rastafari imeiomba serikali kupitia Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo kuhakikisha jamii inarudi katika uhalisia wa mwafrika kwani nchi nyingi zimefanikiwa kwa kufanya historia zao kwa kuzienzi,kuziheshimu na kuzifuata.

Hayo yamezungumza na Mratibu wa matukio maalum Rastafari Mkoa wa Mwanza John Kimori,wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa juu kufanyika kwa tamasha la kutimiza miaka 93 ya Mfalme Haile Selassie wa kwanza tangu kutawazwa na kuwekwa wakfu wa kuwa mfalme wao wa Afrika ambalo litafanyika kitaifa jijini hapa Novemba 2,2023.

“Hayati John Magufuli aliwai kusema kuwa tuandike historia zetu wenye kwaio Mimi nashauri serikali kupitia Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo ijaribu kurudi katika msingi wa Mwalimu Nyerere,Haile Selassie walivyoishi na Nkwame Nkuruma walivyokuwa wakilenga Afrika Union,”ameeleza Kimori.

Sanjari na hayo ametumia fursa hiyo kuwasihi wale wote wanaoweka rasta ambazo siyo asilia(dread rock), kuzingatia na kufuata maadili ya kiafrika pamoja na imani ya Rastafarian, ili kuondoa mtazamo hasi kwa jamii juu ya watu wa jamii hiyo kuwa ni wasiofuata maadili.

Ameeleza kuwa unapofanya kitu jaribu kujua undani wake,usifanye kitu huku hujui undani wake na ukija kuulizwa unajibu kitu ambacho unapotosha ndio maana wanaenda kutoa tamko rasmi la kuweka mfumo wa kimaadili na kila kitu kuhusu jamii ya Rastafari.

“Sisi ni watu huru,tunapenda watu wawe huru tusiwafanye kuwa watumwa kwaio mtu anafanya dreadrock(rasta ambazo siyo asilia) anaweza kufanya vitu vilivyo kinyume na imani yao kama vile kunywa pombe,akagombana na watu akafanya uhalifu,wizi hivyo inatoa picha kuwa rasta ni mhalifu,”,ameeleza Kimori na kuongeza kuwa

“Ninachowaambia kufanya hizo ‘fashion dread’ wajaribu kujua tayari wameenda kuonekana Rastafarian kiimani kwaio anapaswa waende katika maadili,kuishi katika maadili,asiharibu maadili ikaonekana Rasta kavuruga maadili kwa sababu duniani hatuwezi kumzuia mtu na sisi tunafurahi kwa sababu tunaona wanaipenda Rasta na kuhiitaji japo kuwa wanashindwa kuwa na Rasta asilia,hivyo wanapaswa kuwa na tabia njema,wasikivu na kuwa katika maadili ya kiafrika na wasiwadharirishe na kuzani Rasta wanaishi hivyo wafuate maadili tu,”.

Aidha ameeleza kuwa hawakubaliani na uhalifu wowote hivyo wanashirikiana na serikali ikiwemo kuwakanya na kuwakumbusha watu kuacha dhambi,uhalifu na kuzingatia kufanya kazi na kujitegemea kwani wao wanashauri elimu ya kujitegemea kwa sababu Rastafari wengi wanafanya kazi za kujitegemea na maendeleo.

Mwakilishi wa wakinadada Rastafari Tanzania,Masika Kazimoto ameeleza kuwa jamii inapaswa itambue kuwa mwanamke kuwa na rasta siyo kuwa ni muhuni bali wanazingatia maadili.

“Wakinadada wa imani ya Rastafari tupo tofauti na wale wanaofuga tu rasta tunazingatia maadili ya kiafrika na ya jamii yetu maana haturuhusiwi kuvaa nguo fupi,heshima kila mahali,”.

Pia ameeleza kuwa wanashiriki katika shughuli za kijamii na kimaendeleo kwa kufanya biashara mbalimbali, kutengeneza vitu tofauti tofauti.

“Tunaimani kupitia jukwaa la wanawake Rastafarian la maendeleo litakalozinduliwa Novemba 2,mwaka huu kimaendeleo litawasaidi kwani tutakutana na viongozi wa kiserikali na kuwaeleza hivyo tunaimani watatusikia na tutaweza kupata mikopo na kufungua viwanda vidogo kwa sababu uwezo tunao,”.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tanzania Rastafari Movement(TARAMO)Hugo Mambo, ameeleza kuwa wataenda kutoa elimu kuhusu majina ambapo walizaliwa na kupewa majina ya kigeni.

“Hata jina lina nguvu yake ndio maana Rastafari tumerudi katika majina ya babu zetu ndio maana nimeamua kuitwa Rasi Mambo,Mambo ni jina la babu yangu,” ameeleza Mambo.