December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rasmi Chatsoko mdhamini mkuu wa Goba Hills Marathon 2025

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online


Chatsoko, programu maarufu ya FastHub inayotegemea WhatsApp, huwasaidia watumiaji kununua bidhaa kwa urahisi, kufanikisha usajili, na kurahisisha mawasiliano na malipo kupitia simu. Kwa ufadhili huu, Chatsoko inataka kuimarisha uhusiano wake na umma wa Watanzania kwa kuunga mkono tukio pendwa ya kila mwaka kama Goba Hills Marathon, ambayo huvuta maelfu ya washiriki watokao nchini kote.

Marathoni hii, iliyopangwa kufanyika Tarehe 1 Februari 2025,itakayokuwa na washiriki zaidi ya 2000 watakaokimbia Kilomita 5,10,21.1 na 42.2 zitakazoanzia viwanja vya GOBA Sekondari zitaonyesha chapa ya Chatsoko katika kipindi chote cha mbio hizo, kuanzia mwanzo wa mbio hadi mwisho.

Pia, Chatsoko itatoa programu ya usajili itakayowezesha washiriki kujiandikisha na kufanya malipo kupitia WhatsApp.

Zaidi ya hayo, washiriki watapokea jumbe fupi zenye maelezo ya wapi wanaweza kwenda kuchukua vifaa vya kukimbilia na maelezo muhimu kuhusu eneo husika kwa ajili ya siku ya marathoni.

Mkuu wa Mauzo wa Fasthub, Christine Abulitsa, alitoa maoni kuhusu udhamini huo, akisema:
“Tunafurahi kudhamini Mbio za Goba Hills za 2025 kupitia Chatsoko. Ushirikiano huu unaendana na dhamira yetu ya kutoa suluhisho za kidijitali bunifu zinazowapa watumiaji wetu uzoefu usio na dosari. Chatsoko itatoa jukwaa rahisi la usajili ambapo washiriki wanaweza kujisajili kwa urahisi kwa mbio na kufanya malipo. Tunatarajia kuboresha urahisi na ushirikishwaji wa uzoefu wa mbio hizi.”

Mwenyekiti wa Goba Roads Runners Revocatus Kahendaguza amesema“Goba Hills Marathon ni mbio kubwa sana Tanzania, Imeendeshwa kwa misimu mitano mfululizo na msimu huu ni wa sita ambao utakuwa wakipekee sana.Maandalizi yote ya msingi yamefanyika ikiwemo kit bora na za kisasa lakini zaidi ya yote mfumo wa Chatsoko utawezesha watu wengi sana kusajiri.Goba Hills Marathon imeifikia jamii kwa kipindi chote tangu kuanza kwake, kwa msimu huu tutawafikia kwa namna tofauti. Kupitia mbio hii tunaenda kuanzisha program maalumu za afya mashuleni yote ni katika kuboresha maisha kupitia mbio.Tunawaalika wadau mbalimbali kushiriki nasi CHATSOKO GOBA HILLS MARATHON 2025”