Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
WAZIRI wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amesema,Rasimu ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014,toleo la 2023 imekamilika huku akiwataka wadau wa Elimu kutoa maoni ya mwisho kwa ajili ya kupata Sera kamili .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Mei 09 ,2023 Prof.Mkenda amesema kazi hiyo imekuwa ikifanyika kwa kukusanya maoni ,kutembelea nchi mbalimbali na kufanya uchambuzi wa kitaalam.
“Ninayo furaha kuwajulisha kuwa rasimu ya sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014 toleo la 2023 imekamilika,kadhalika Rasimu ya Mitaala mipya ya elimu ya Awali ,msingi,sekondari na vyuo vya ualimu ambayo inakidhi maelekezo ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan nayo imekamilika.”amesema Prof.Mkenda na kuongeza kuwa
“Serikali imeamua kutoa Rasimu hizo hadharani ili kupata maoni ya mwisho na tungependa kuyapokea maoni hayo ifikapo Mei 31 mwaka huu.”
Amesema kutakuwa na kongamano la siku tatu la Sera na Mitaala ya Elimu litakalofanyika jijini Dodoma kuanzia mei 12 hadi 14 mwaka huu ambao wadau wa elimu kwa pamoja watakutana ili kutoa maoni yao .
Vile vile amewaasa wananchi kutolea maoni rasimu hizo ambazo amesema baada ya kuzingatia maoni ,Srikali itaingiza kwenye michakato ya maamuzi.
Kwa mujibu wa Prof.Mkenda ,Wizara imeandaa semina kwa wabunge ili iwapitishe kwenye rasimu hizo ili nao waweze kutoa maoni yao kwa mustakabali wa Taifa kwa ujumla.
“Rasimu zote zinapatikana kwenye kwneye Tovuti ya Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Idara ya Habari Maelezo na Idara ya Taasisi ya Elimu Tanzania.”amesema Prof.Mkenda
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Caroline Nombo amesema,wananchi wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) nao watapata fursa ya kutoa maoni yao kwa kutumia utaratibu maalum uliowekwa ajili yao.
More Stories
Serikali ya Kijiji Ilungu yawakatia bima za afya wananchi 1500
TMA kuendelea kufuatilia mifumo yake
Wassira:Waliopora ardhi za vijiji warudishe kwa wananchi