Na Moses Ng’wat,Timesmajiraonline,Songwe.
KATIBU Tawala wa Mkoa (RAS) wa Songwe, Happiness Seneda, ameongoza hafla ya kukabidhi mablanketi kwa watoto yatima, watoto waishio katika mazingira hatarishi, na wazee wasiojiweza.
Msaada huo wa mablanketi 924 umetolewa na Shirika la Lutheran World Relief (LWR) kwa kushirikiana na Shirika la Actions for Development Programs-Mbozi (ADP-MBOZI). Hafla hiyo imefanyika leo Februari 28, 2025, katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Songwe.
Akizungumza katika hafla hiyo, Seneda aliwashukuru wahisani kwa msaada huo, akisema utaimarisha ustawi wa makundi yenye uhitaji. Pia alisisitiza umuhimu wa kushirikiana na wadau wa maendeleo ili kuendelea kusaidia wananchi, hasa katika maeneo yenye changamoto zaidi.
Msaada huo wa mablanketi utasambazwa katika halmashauri na vituo mbalimbali ndani ya mkoa wa Songwe. Wilaya ya Ileje itapatiwa belo 4, Mbozi 7, Momba 4, Songwe 5, na Halmashauri ya Mji Tunduma belo 4. Vituo vilivyonufaika ni pamoja na Kituo cha Yatima cha Hospitali ya Isoko (belo 2), Kituo cha Mbozi Mission (belo 1), na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe (belo 1).
Seneda alihitimisha kwa kuhimiza wadau wa maendeleo kuendelea kushirikiana na serikali katika kuinua hali ya maisha ya makundi yenye uhitaji mkoani Songwe.



More Stories
The Desk and Chair yatoa vifaa saidizi kwa Masatu na mkewe
jengo la mama,mtoto la bilioni 6.5 lazinduliwa Mbulu
Dkt.Malasusa ataka hospitali ya Haydom kuombea wafadhili wanaoishika mkono