Mary Margwe, Timesmajira Online,Babati
Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara,Maryam Muhaji, amemuomba Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Utawala ya Bodi ya Wakurugenzi RUWASA Prof. Aloyce Mvuma, kutoa kipaumbele ukamilisha ujenzi wa bwawa la kimkakati la Dongo llililopo wilayani ya Kiteto itakalohudumia Mikoa mitatu ikiwemo Manyara.
Muhaji ameyasema hayo Februari 12,2025,wakati wa ziara ya Mwenyekiti huyo ya kukagua majaribio ya mita za maji Kata ya Gidas wilayani Babati mkoani humo, ambapo amesema bado Kuna uhitaji wa maji katika Wilaya zote za Mkoa huo.
![](https://timesmajira.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250214-WA0013-1024x640.jpg)
Hivyo kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa bwawa la kimkakati la Dongo litasaidia kuhudumia vijiji 20 vya Wilaya ya Kiteto, Gairo mkoani Morogoro na Kongwa mkoani Dodoma.
“Usanifu wa bwawa la Dongo umekamilika, naomba ujenzi wake upewe kipaumbele hasa kwenye bajeti hii ya 2025 / 2026,”amesema Katibu Tawala huyo.
Sanjari na hayo amesema suala jingine la kupewa kipaumbele ni kuiwezesha RUWASA Mkoa wa Manyara vyombo vya usafiri,kwani imepata changamoto katika kutekeleza majukumu yao,na wakati mwingine wanalazimika kuazima vyombo hivyo katika Wilaya ya Simanjiro na Hanang.
Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Utawala ya Bodi ya Wakurugenzi RUWASA Prof. Aloyce Mvuma,amesema bodi hiyo itahakikisha kuwa mradi huo unakua endelevu na msaada zaidi kwa jamii ili kufikia matamanio ya utoaji huduma ya maji kama ilivyopangwa.
Awali Meneja wa RUWASA Mkoa wa Manyara,James Kionaumela, amesema upatikanaji wa maji katika Mkoa huo ni asilimia 75.5,ambapo Wilaya ya Babati inaongoza kwa upatikanaji wa maji kwa asilimia 80.9 ,Kiteto asilimia 64, Simanjiro 66.7, Hanang’ 71.2 na Mbulu 69.7 sawa na ongezeko la asilimia 14.7% kutoka Juni 2019 mara ilipoanzishwa RUWASA.
“Mkoa wa Manyara una jumla ya vijiji 440 kati ya hivyo vijiji 396 vinahudumiwa na RUWASA huku 44 vikihudumiwa na Mamlaka za Maji na Usafi wa Mzingira.Ambapo vijiji vinavyohudumiwa na RUWASA,vijiji 329 vina huduma ya maji kati ya hivyo vijiji 277 maji ya mtandao na 52 pump za mkono na solar huku vijiji 67 havina huduma ya maji ya uhakika,”amesema.
![](https://timesmajira.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250214-WA00151-1024x640.jpg)
Hadi kufikia Desemba 31, 2024 upatikanaji wa maji katika Wilaya ya Babati asilimia 80.9, Kiteto asilimia 64, Simanjiro asilimia 66.7, Hanang’ asilimia 71.2 na Mbulu asilimia 69.7 sawa na ongezeko la asilimia 14.7% kutoka Juni 2019.
Kionaumela,amesema wakazi wanaohudumiwa na RUWASA ni zaidi ya milioni 1.5,wenye maji ni milioni 1.06, ambao hawana maji ya uhakika ni watu 478,902 huku wastani wa uzalishaji wa maji kwenye Skimu 209 ni lita zaidi ya milioni 42.7 kwa siku.
![](https://timesmajira.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250214-WA0014-1-1024x640.jpg)
More Stories
Kapinga ashiriki kikao cha Mawaziri wa kisekta Arusha
TCB yawazawadia washindi wa kampeni ‘Mahaba Kisiwani’
Mwakagenda:Zao la ndizi liuzwe katika masoko ya kimataifa