December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rapper Black Rob afariki dunia

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

RAPPER maarufu wa New York nchini Marekani ambae aling’aa sana chini ya Lebo ya Bad Boy, Robert Ross maarufu kama ‘Black Rob’ amefariki dunia kutokana na tatizo la figo.

Kwa mujibu wa Mitandao ya Marekani umeripoti kuwa Rob amefariki akiwa na umri wa miaka 51 ikiwa ni ndani ya siku 10 tu tokea Rapper mwingine wa New York Earl Simmons ‘DMX’ kufariki akiwa na umri wa miaka 50.

Rob alikulia East Harlem, New York na kuanza kuwa karibu na Label ya Bad Boy ya Diddy mwanzoni mwa 1996 na kutokea kwenye featuring kama za ‘come see me’ remix ya 112, ‘love like this’ ya Faith Evans na nyingine.

Mwanzoni mwa miaka 2000 aliachia ‘whoa!’ ambayo ilikua ‘smash hit’ iliyomuingiza kwenye Top 10 ya R&B/Hiphop bora za wakati huo na inatajwa kuwa ‘solo single’ pekee iliyowahi kumuingiza kwenye 100 bora za chati ya Billboard.