Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Rais wa Chama cha Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Matibabu ya Fistula Dkt. James Chapa (Kulia kwa Mhe Waziri) ameongoza timu ya wataalamu mabingwa wa fani hiyo akiwemo Dkt. Mtinangi na Dkt. Haule kuonana na Waziri wa Afya kujitambulisha na kuomba ushirikiano katika kuwezesha programu ya matibabu ya Fistula inayotekelezwa na Chama hicho kwa ushirikiano na Wizara ya Afya na wataalamu toka nje ya nchi MMS Foundation Canada ambao Septemba 2021 waliweka kambi mkoani Katavi na kuwezesha kufanya upasuaji kwa wanawake wenye matatizo ya fistula mkoani humo. Lengo ni kuwafikia akina mama wengi zaidi nchi nzima.
Dkt Gwajima amewapongeza wataalamu hao kwa moyo wa uzalendo na amewahakikishia kupata ushirikiano wote Ili wapanue huduma yao na kuwafikia wananchi wengi zaidi.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua